Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alhamisi ilikuwa mwisho wa dirisha la usajili wa Januari huko England na makocha wengi walikuwa bize kwenye kufanya maboresho kwenye vikosi vyao.
 
Kinapofika kipindi cha usajili, kuna makocha hao wamekuwa maarufu kwa kuuza kuliko kununua, lakini wengine wamekuwa kinyume chake, wananunua kuliko kuuza. Kwa takwimu zilizonaswa huko Ulaya ni kwamba kuna makocha watano ndio walioziingizia klabu zao pesa nyingi sana kutokana na kuwapiga bei wanasoka mastaa. Hii hapa ndio orodha ya makocha walioingiza mamilioni kwa kuuza wachezaji mastaa.
 
5.Unai Emery-Pauni 466.61 milioni

Kocha wa Arsenal, Unai Emery ni mmoja wa makocha waliopiga pesa nyingi kwa kuuza mastaa wao. Katika maisha yake ya ukocha, Mhispaniola huyo ameuza jumla ya wachezaji 59 katika klabu tano alizowahi kuzinoa. Kwenye mauzo ya wachezaji hao, Emery ameingiza kiasi cha Pauni 466.61 milioni.
 
Lakini, kwenye klabu yake ya sasa Emery, Arsenal wanahitaji kununua zaidi kuliko kuuza, hivyo pengine mkwanja huo alioingiza kwenye timu anazonoa, utabaki kwa muda mrefu kwenye kikosi hicho kwa sababu Arsenal kwa sasa wanahitaji kufanya usajili kuboresha kikosi chao kuliko kuuza, licha ya kuwapo kwa ripoti kwamba supastaa Mesut Ozil anaweza akapigwa bei.
 
4.Diego Simeone- Pauni 494.43 milioni

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefundisha klabu nne katika maisha yake ya soka. Katika kipindi chake hicho cha ukocha kwenye vikosi hivyo, kocha huyo Muargentina amepiga bei jumla ya wachezaji 54 kwa thamani ya Pauni 494.43 milioni. Katika kipindi hicho cha klabu nne alikopita, kocha huyo amebeba mataji saba.
 
Kutokana na kuingiza pesa nyingi hivyo, Simeone anaingia kwenye orodha ya makocha mahiri huko Ulaya ambao waliingiza mkwanja wa kutosha kutokana na kupiga bei masupastaa kibao kwenye vikosi vyao walivyowahi kuzinoa.
 
3.Jose Mourinho- Pauni 510.59 milioni

Kocha Mreno, Jose Mourinho kwa sasa yupo tu mtaani hana kazi tangu alipoachana na Manchester United, Desemba mwaka jana. Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Inter Milan na Real Madrid kwenye maisha yake ya soka ameuza wachezaji 64 na kuingiza kiasi cha Pauni 510.59 milioni.
 
Wakati alipokuwa kwenye kikosi cha Chelsea huko Stamford Bridge, Mourinho aliingizia timu hiyo pesa nyingi kutokana na kuuza wachezaji pengine imekuwa hivyo kwa sababu ndipo mahali alipodumu kwa muda mrefu katika awamu zake mbili alizokuwa kwenye timu hiyo.
 
Kutokana na hilo, kocha Massimiliano Allegri atakuwa kwenye presha kidogo kwa sababu kikosi chake kimejengwa vyema, lakini bado anapoteza fursa za kunyakua mataji kwa msimu huu. Katika kibarua chake hicho cha ukocha, Allegri, aliyewahi pia kuinoa AC Milan, amepiga bei wachezaji 100 na kuingiza Pauni 595.59 milioni.
 
1.Leonardo Jardim- Pauni 785.66 milioni

AS Monaco kwao muda umekwenda kwa kasi sana. Msimu wa 2016/17 walikuwa mabingwa wa Ulaya, lakini msimu huu wa 2018/19 wanapambana na hali yao wasishuke darasa. Wapo kwenye nafasi ya 19 na pointi zao 15.. Henry ameondoka na Jardim amerudi tena kwenye kiti.
 
Jardim ndiye kocha aliyevuna pesa nyingi kwa kuuza wachezaji wengi huko Ulaya kwa sasa. Mastaa waliouzwa na kocha huyo ni pamoja na Kylian Mbappe (PSG), Bakayoko (Chelsea), Benjamin Mendy (Man City), Silva (Man City), Fabinho (Liverpool) na Thomas Lemar wa Atletico Madrid na ameiingioza Pauni 785.66 milioni.
 
Jumapili ya furaha
IMG_20190128_130732.jpeg
 
Back
Top Bottom