Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3d85540b-51ca-40f3-92bb-a4d09f6770e3.jpeg
 
Najaribu kuangalia mchango wa:

1.Nicolas Gyan
2.Juuko Murshid
3.Paschal Wawa
4.Cletus Chama
5.Medie Kagere
6.James Kotei
7. Emmanuel Okwi
8. Ahsante Kwasi

Hivi ni kweli wanaisaidia Simba? Ina Mana wachezaji wetu wa kitanzania wasingeweza kufungwa hizo 5 Hadi tunakodi wachezaji wa kigeni waje kufungwa hizo?
 
*NCHI IMEFEDHEHESHWA*

[emoji2398] *Dr Beatus Chikoti*

1. Mwana kalilia wembe,
watu wakampatia
Kajipachika ubembe,
fedheha kajitwalia
Amekinywea kikombe,
makaa kajipalia
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

2. Waliuanza kwa kasi,
Ahli kushambulia
Sulaya yule kwa kasi,
moja akajipigia
Yalikuwa ni matusi,
Wahed kuhesabia
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

3. Ithnan likafuata,
Maaluli katupia
Konzi akawakong'ota,
waomboleza mikia
Kimya wakajikunyata,
kwa hofu wajililia
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

4. Ajayi yule mahiri,
la tatu kawatungua
Alifunga kijasiri,
thalatha yakatimia
Sasa haikuwa siri,
kuwa simba kapotea
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

5. Walisikitisha Simba,
wanaoitwa mikia
Hawakuweza kukaba,
iliwaishia nia
Yakatimia arba,
manne nakuambia
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

6. Wahid hakuridhika,
la nne kuwafungia
La tano akapachika,
khamsa yakatimia
Ilikuwa hekaheka,
mkono kujirudia
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

7. Yote hayo yalijiri,
kipindi cha kuanzia
Waliitafuta shari,
nayo ikawaendea
Walijifanya hodari,
wakati wamelegea
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

8. Kwenye michezo miwili,
asharah wamechezea
Hawawezi fika mbali,
Pamoja na kukamia
Imewaishia hali,
watamani kukimbia
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

9. Parachichi walipakwa,
awali nawaambia
Ndiyo maana wamebakwa
Khamsa zikatimia
Kisha wakasukwasukwa,
Kibla kuelekea
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.

10. Simba muache kiburi,
aibu mmetutia
Mlileta ujeuri,
ngebe wamewakatia
Mmevunjwavunjwa ari,
Tanganyika inajua
Nchi imefedheheka,
kwa sababu ya mikia.
 
Back
Top Bottom