Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Baba kipanga
20190207_211011.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu ya Manchester City imerejea kileleni kwa mara nyingine kwenye msiamo wa Ligi Kuu England baada ya kuifunga Everton mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Godson Park jana jumatano usiku.
 
Dalili za Manchester City kurejea kileleni zilianza kuonekana wiki hii baada ya Liverpool kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham, jambo ambalo liliongeza presha kwa kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp.
 
Kwa ushindi huo, umeziingiza vitani timu za Liverpool na Man chester City kipindi hiki cha msimu kilichobaki kwa kuwa zitakuwa zinafukuzana kukaa kileleni.
 
Manchester City wapo kileleni wakiwa na alama 62 huku wakifuataiwa na Liverpool wakiwa napointi 62 lakini wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
 
.JANA Manchester City ilikuwa inatarajiwa kuongoza Ligi Kuu ya England kama ingezoa pointi zote tatu ugenini kwa Everton. Kisa? Liverpool imeshusha kasi yake na kuanza kupoteza pointi mfululizo tofauti na hapo awali.
 
Jumatatu Liverpool kwa mara ya pili ilitoka sare na West Ham ikiwa ni baada ya kutoka sare ya awali dhidi ya Leicester City. Na sasa imebainika kwamba kikosi cha kocha, Jurgen Klopp kinateseka na majeraha ya wachezaji wengi kikosini.
 
Walinzi watatu muhimu katika kikosi cha kwanza Trent Alexander-Arnold, Dejan Lovren na Joe Gomez pamoja na viungo wawili, Jordan Henderson na Georginio Wijnaldum wote walikosa safari ya London kucheza dhidi ya West Ham.
 
Timu inafanya vema kwa sasa na tuna kipindi kigumu. Majeraha. Sijui yanatokea wapi au ugonjwa. James Milner alikuwa mgonjwa, na inawezekana ni mgonjwa mpaka sasa.
 
Na Virgil van Dijik alikuwa nje kwa siku au nne kabla ya mechi. Amepoteza kilo tatu au nne. Hali hii haisaidii. Ni hali ngumu kwa vijana lakini bado wanapambana,” alisema Klopp.
 
Silalamiki sana kuhusu hilo isipokuwa nasema kweli. Sio kisingizio. Milner alirudi uwanjani lakini jana (juzi) alishindwa kufanya mazoezi. Alikuja London peke yake kwa sababu alikuwa anaumwa. Hiyo sio sahihi kwakweli.” Alisema Klopp.
 
Mwezi mmoja uliopita Liverpool walikuwa wakifurahia kujitanua kileleni lakini mwanzoni mwa Januari walipoteza pambano lao la kwanza la Ligi Kuu dhidi ya Manchester City kabla ya kutolewa na Wolves katika kombe la FA na kisha sare hizi mbili mfululizo dhidi ya Leicester City na West Ham.
 
Hali hii imeanza kupunguza uwezo wao wa kujiamini kuelekea katika kutwaa taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya England tangu mwaka 1990 na sare dhidi ya West Ham inamaanisha kwamba City na Tottenham sasa ni tishio katika mbio za ubingwa.
 
Back
Top Bottom