Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pambano hilo dhidi ya West Ham pia lilionyesha kwamba staa James Milner hawezi kutegemewa kuwa mlinzi wa kulia huku miguu yake ikianza kuchoka kutokana na umri lakini wakati walinzi wengine wanaoweza kucheza nafasi hiyo Alexander-Arnold na Gomez wakiwa majeruhi, imeshangaza kuona Liverpool wamemtoa kwa mkopo mlinzi, Nathaniel Clyne kwenda Bournemouth kwa mkopo.
 
Kukosekana kwa Henderson na Wijnaldum kulisababisha Adam Lallana acheze mechi hiyo katika eneo la kiungo ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuanza tabu Oktoba mwaka jana na Lallana licha ya kushiriki kutengeneza bao la Sadio Mane lakini alionekana kutokuwa na makali katika eneo hilo.
 
Wakati huo huo, kiungo wa kimataifa wa Brazil Fabinho alishindwa kuwa na kasi ambayo Henderson au Wijnaldum wanayo. Naby Keita alichemsha katika pambano hilo huku akizimwa vema na viungo wa West Ham, Mark Noble na Declan Rice.
 
Safu ya ulinzi ya Liverpool kwa mara nyingine tena timu hiyo ilishindwa kuzuia nyavu zake zisigugwe licha ya kutamba zaidi katika safu ya ulinzi mwanzoni mwa mwaka huu. katika mechi 19 za mwanzo Liverpool ilizuia mechi nane kati ya 12 nyavu zao zisiguswe. Kwa sasa wamefungwa mabao saba katika mechi sita zilizopita.
 
Kukosekana kwa Alexander-Arnold na Lovren kunaiumiza Liverpool wakati mlinzi, Joel Matip ameshindwa kutengeneza kombinesheni imara na mbabe Van Dijk.
 
Habari njema kwa Klopp ni kwamba watu wake watatu muhimu katika safu ya ushambuliaji, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Mane wameendelea kubakia kuwa fiti.
 
Watatu hao wamefunga mabao nane katika mechi zaoi tano tangu mwaka 2019 uingie lakini hata hivyo staa wa Manchester City, Sergio Aguero anaonekana kuwa moto zaidi baada ya kufunga mabao matano katika mechi tano za mwaka huu ikiwemo Hat trick aliyopiga dhidi ya Arsenal.
 
Hata hivyo, Salah, Mane na Firmino, ndio wachezaji pekee ambao wameifungia Liverpool mabao tangu mwaka 2019 uingie na ni vema kusema kwamba wamekuwa wakitimiza jukumu lao vema lakini safu ya ulinzi imekuwa ikiwaangusha.
 
Malcom alifunga bao la kusawazisha na kuisaidia Barcelona kupata sare dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Mfalme kwenye Uwanja wa Nou Camp.
 
Mabingwa watetezi Barcelona walianza bila ya nyota wao Lionel Messi, ilishindwa kuonyesha ubora wao katika kushambulia pamoja na jitihada za Malcom.
 
Bao la Mbrazili huyo limeifanya mechi ya marudiano itakayofanyika kwenye Uwanja wa Bernabeu Februari 27 kuwa na hisia ya aina yake.
 
Barcelona inayosaka taji la tano mfululizo la Kombe la Mfalme ilipoteza umakini katika safu yake ya ushambuliaji kutokana na kukosekana kwa Messi aliyekuwa benchi baada ya kuumia hivi karibuni.
 
Naye Gareth Bale alikiwa benchi kwa upande wa Real hivyo kutoa mwanya kwa chipukizi wawili wa Brazil, Vinicius Junior (18) wa Real na Malcom (21) wa Barca kuonyeshana ubabe.
 
Katika La Liga Jumamosi hii Real watakuwa na kibarua dhidi ya Atletico Madrid wakati vinara Barcelona watakuwa ugenini Jumapili kuivaa Athletic Bilbao.
 
Mshambuliaji huyo wa Argentina, Sala pamoja na rubani wake David Ibbotson wakiwa katika ndege aina ya Piper Malibu N264DB walipata ajali baada ya ndege hiyo kupotea katika rada karibu na Guernsey, Januari 21.
 
Sala (28), alivunja rekodi ya uhamiso wa Cardiff, lakini hajapata nafasi ya kuichezea klabu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…