Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni nani huyu Denis Suarez?

Azaliwa Hispania, aibukia Man City. Jina lake kamili ni Denis Suárez Fernández na alizaliwa katika kitongoji cha Salceda de Caselas nchini Hispania mnamo Januari 6, 1994. Alianza kucheza soka katika klabu za vijana za Porrino na kisha Celta Vigo.
 
Kutokana na kiwango kizuri ambacho alionyesha, Suarez alianza kuandamwa na klabu mbalimbali kubwa za Ulaya lakini walikuwa Manchester City ambao waliinasa saini yake mnamo Mei 23, 2011. Kwa kuinasa saini yake, City ilikuwa imezipiga bao klabu za Barcelona, Chelsea na Manchester United ambazo zilionyesha nia ya kumchukua.
 
City walilipa dau la Pauni 850,000 huku kukiwa na uwezekano wa pesa hizo kuongezeka mpaka Pauni 2.75 milioni kutokana na kiwango chake na idadi ya mechi ambazo atakuwa amecheza. Alicheza mechi ya kwanza katika pambano la maandalizi ya msimu mpya wa 2011–12 dhidi ya Los Angeles Galaxy akiingia dakika ya 88 kuchukua nafasi ya Edin Dzeko.
 
Akakaa benchi katika pambano la kombe la Ligi dhidi ya Birmingham City na kisha kucheza mechi yake ya kwanza ya ushindi katika ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Wolves Kombe la Ligi akiingia uwanjani katika dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Samir Nasri.
 
Akakaa benchi katika pambano la kombe la Ligi dhidi ya Birmingham City na kisha kucheza mechi yake ya kwanza ya ushindi katika ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Wolves Kombe la Ligi akiingia uwanjani katika dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Samir Nasri.
Hii avatar mpya hii inanikonfyuzi dah! Haijakaa kirolo modo kabisa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Jamani. Hata wewe the polaiti wani unatufanyia hivi kweli? Timu Tecno kujeni huku kuna mtu anatubipu [emoji16][emoji16][emoji16]

Capital akiona hii na timu yake ya roho mbaya dhidi ya TECNO akiona hii atafurahi balaa....
Hahaha ngojea nitoke nduki kabla hawajaja [emoji2088][emoji2088][emoji2088]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…