KIPA:
Petr Cech
Man United ilisajili makipa kibao kabla ya kumnasa Edwin van der Sar kutoka Fulham. Lakini, kwenye kipindi chao cha kusajili, Ferguson alitaka kumsajili kipa Petr Cech. Ferguson alifunga safari kwenda kumtazama Cech akicheza Rennes mwaka 2003, lakini baadaye alimwona kuwa bado kipa mwenye umri mdogo sana wa kuhimili vurugu za washambuliaji wa Ligi Kuu England. Kutokana na hilo, Fergie akaachana na mpango wa kumsajili kipa huyo kabla ya kuja kutamba England akiwa na kikosi cha Chelsea kabla ya sasa kuitumikia Arsenal kwenye ligi hiyo akiwa na kiwango bora kabisa.