Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo, si kila mchezaji ambaye Ferguson alimtaka basi alifanikiwa kumsajili, kwani kuna mastaa wengine kibao wanaoweza kutengeneza Kikosi cha Kwanza waligoma kunaswa na kocha huyo na hivyo Man United ilikosa huduma zao. Hiki hapa kikosi cha kwanza pamoja na wachezaji wa akiba ambao Ferguson alishindwa kuwasajili licha ya kuwafukuzia na kutamani huduma zao.
 
KIPA:

Petr Cech

Man United ilisajili makipa kibao kabla ya kumnasa Edwin van der Sar kutoka Fulham. Lakini, kwenye kipindi chao cha kusajili, Ferguson alitaka kumsajili kipa Petr Cech. Ferguson alifunga safari kwenda kumtazama Cech akicheza Rennes mwaka 2003, lakini baadaye alimwona kuwa bado kipa mwenye umri mdogo sana wa kuhimili vurugu za washambuliaji wa Ligi Kuu England. Kutokana na hilo, Fergie akaachana na mpango wa kumsajili kipa huyo kabla ya kuja kutamba England akiwa na kikosi cha Chelsea kabla ya sasa kuitumikia Arsenal kwenye ligi hiyo akiwa na kiwango bora kabisa.
 
Carlos alidai kwa kipindi hicho alikuwa na mkataba katika kikosi hicho cha Bernabeu na alikuwa na furaha kubwa, hivyo hakuona sababu yoyote na kuanza kuzungumza na klabu nyingine huku akisema klabu yake na Man United wao kama wanataka biashara hiyo ifanyike, basi watakaa huko na kumalizana wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…