Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Raphael Varane

Kocha, Ferguson alimtaka Mfaransa na beki wa Real Madrid, Raphael Varane, tangu kipindi hicho alipokuwa akiichezea Lens. Kocha huyo alisema mwaka 2011, alipanda treni kutoka Euston hadi Lille kwenda kufanya mchakato wa kumsajili Raphael Varane. Mambo yalikuwa safi kwa wakati huo na mazungumzo na Lens yalikuwa kwenye hatua nzuri, lakini balozi wa Real Madrid, Zinedine Zidane alishtukia dili kwamba Man United wanamtaka Varane, hivyo akafanya kila aliloweza kuhakikisha beki huyo wa kati anakwenda kusajiliwa na Real Madrid na Man United ikagonga mwamba. Ferguson alisema hata Jose Mourinho hajawahi kumwona Varane akicheza, aliletewa tu mchezaji kwenye kikosi.
 
Paolo Maldini

Ferguson aliwahi kusema, alipambana kwa nguvu zote kutaka kumsajili, Paolo Maldini, lakini ashindwa kumng’oa supastaa huyo kutoka AC Milan. Kocha huyo wa Man United wa kipindi hicho alisema alipomfuata baba yake Paolo, Cesare, alikutana na majibu ya kutikisiwa kichwa tu, kabla ya kupewa majibu ya mdomo, yaliyomkatisha kabisa tamaa ya kumpata beki huyo.
 
Javier Zanetti

Beki Muargentina, Javier Zanetti ni moja ya wachezaji waliovumishwa sana kwamba alikuwa anakaribia kabisa kujiunga na Man United, lakini dili hilo lilishindwa kukamilika. Mchezaji huyo anadai alikutana na Ferguson mara kadhaa na kocha huyo alikuwa akimpiga maneno kwamba aende akajiunge na Man United, lakini aliona abaki na msimamo mmoja tu wa kubaki kwenye kikosi cha Inter Milan licha ya kipindi hicho mambo yao yalikuwa hovyo ndani ya uwanja na Man United walikuwa juu sana kisoka. Zanetti alisema hawakuwa Man United tu waliotaka kumsajili, kulikuwa na klabu nyingine kubwa kadhaa, lakini mapenzi yake na Inter yalizidi mizani ya timu nyingine zote zilizomtaka.
 
VIUNGO

Ronaldinho

Ferguson alipigwa kikumbo na Barcelona kwenye usajili wa Mbrazili, Ronaldinho. Kilichotokea ni Man United ilikaribia kunasa huduma ya kiungo huyo mshambuliaji mwaka 2003 kipindi hicho akiwa PSG, kabla ya Barcelona kuja juu na kumchukua supastaa huyo fundi wa mpira.
 
Ronaldinho mwenyewe alisema alibakiza saa 48 tu kwenda kusaini kujiunga na Man United, lakini Sandro Rosell aliwawahi Man United kwa kumwaambia mchezaji huyo kama atachaguliwa na Barcelona kuwa rais basi atakwenda kumsajili kwa sababu hiyo ilikuwa ahadi aliyotoa huko kwenye kampeni zake Nou Camp baada ya kushindwa kunasa huduma ya David Beckham.
 
Michael Essien

Man United ilikuwa na nafasi ya kumsajili Michael Essien miaka minane nyuma kabla ya Chelsea kwenda kuinasa huduma yake mwaka 2005.

Kipindi hicho kiungo huyo wa Ghana alikuwa akiichezea FC Bastia, lakini Ferguson alijivutavuta na kumfanya staa huyo kwenda kujiunga na Olympique Lyon ambako ndiko hasa The Blues walikoenda kunasa huduma yake baada ya kuwa chini ya Jose Mourinho. Essien alikuja kumenyana mara kadhaa na Man United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwenye Ligi Kuu England na makombe mengine na bila ya shaka, Ferguson alisoma namba kwa kupuuza kumsajili staa huyo.
 
Zinedine Zidane

Ferguson aliamua kumsajili Eric Cantona mwaka 1996 na kuachana na mpango wa kunasa huduma ya Mfaransa mwingine, Zinedine Zidane. Kocha huyo alikuwa na nafasi ya kumsajili Zidane kipindi hicho alipokuwa kwenye kikosi cha Bordeaux, lakini kocha huyo aliyeacha historia kubwa huko Man United, alimwona mchezaji huyo anacheza kwenye nafasi sawa anayocheza Eric, ambaye alimwona bora kwa wakati huo kuliko Zidane. Fergie alitaka kwenda kumsajili tena Eric, hivyo aliona kama atamchukua pia Zidane atakuja kuleta shida kwenye nafasi ya kumtumia Eric, hivyo aliamua kuachana na Zidane na kufanya ishu moja ya Cantona.
 
Gareth Bale

Man United ilikuwa na nafasi ya kumsajili Gareth Bale kipindi hicho akiwa mdogo na alikuwa akicheza beki ya kushoto huko kwenye kikosi cha Southampton. Lakini, wakati Ferguson akijiuliza aende kumsajili Bale au aache, Tottenham ilifanya kweli ikaenda na Pauni 5 milioni na kunasa huduma ya mchezaji huyo kama beki wa kushoto kabla ya kuja kubadilishwa na Kocha Harry Redknapp akimchezesha kiungo wa kushoto na tangu hapo akawa staa mkubwa na kusajiliwa kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia Pauni 85 milioni huko Real Madrid. Alipotajiwa ada ya Pauni 5 milioni, Ferguson aliona kubwa sana.
 
WASHAMBULIAJI

Ronaldo

Sir Alex Ferguson aliwahi kudai klabu ya Man United ilihangaika kunasa huduma ya straika mmoja mkubwa katika historia ya soka na huyo si mwingine alikuwa Mbrazili, Ronaldo de Lima.

Fergie alisema “Tulitaka kumsajili straika mmoja wa Kibrazili kutoka Cruzeiro mwaka 1994, lakini tulikwama kupata kibari cha kazi, hivyo alikwenda PSV Eindhoven.” Ingekuwaje kama Fergie angempata Ronaldo na kucheza kwenye kikosi chake, mtu ambaye baadaye alikuja kuwapa tabu sana uwanjani Old Trafford akiwa na Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…