Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kaka

Ferguson alijaribu kumsajili Kaka na ndugu yake, Digao, wakati huo walipokuwa wadogo na wanatamba huko AC Milan. Mbrazili huyo, Kaka alicheza kwenye kikosi cha Milan kwa mafanikio makubwa sana na kuitesa Man United ya Ferguson mara kadhaa kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kwenda zake Real Madrid, kisha akarudi tena Milan na kurudi kwao Brazil.

Kaka mwenyewe aliwahi kusema kuhusu Ferguson: “Kuna wakati alitaka kunisajili mimi na kaka yangu tukiwa Milan, lakini tuliamua kubaki.”
 
Wachezaji wengine

Kwenye orodha ndefu ya wachezaji ambao Ferguson alitamani kuwa na huduma zao kwenye kikosi cha Man United na kujaribu kuwasajili bila ya mafanikio ambapo kwa sasa angekuwa na rekodi ya kuwanoa masupastaa wa maana sana kwenye soka la dunia ni pamoja na Raul, Paul Gascoigne, Didier Drogba, Sergio Aguero, Thomas Muller, Alan Shearer na Frank Lampard.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…