Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki wa pembeni raia wa Ufaransa Faitout Maouassa, 20, hakuwa tayari kujiunga na klabu ya Newcastle mwezi uliopita lakini amesema ni ndoto yake kuchezea Ligi ya Premia siku moja. (L'Equipe via Newcastle Chronicle)
 
Miamba hiyo ya Serie A wanatarajiwa kufanya mazungumzo na kiungo wa Real Madrid Isco, 26, ama kiungo raia wa Colombia James Rodriguez, 27 - ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo na Munichfrom Real - ili kuziba pengo la mshambuliaji raia wa Argentina forward Paulo Dybala, 25, endapo atahama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Tuttosport)
 
Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anasisitiza kulipwa mashahara wa £350,000 kwa wiki ambazo zitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi nyuma ya Alexis Sanchez anayelipwa £400,000 kwa wiki . (Mirror)
 
Barcelona inafikiria kuimarisha safu yao ya ulinzi ya kushoto na sasa wanamlenga beki wa Lyon Ferland Mendy, 23, Filipe Luis, 33, wa Atletico Madrid na kinda anayelengwa na Real Betis Junior Firpo, 22,. (Mundo Deportivo)
 
Uamuzi wa Beki wa Ajax Matthijs De Ligt wa kujiunga na ajenti maarufu Mino Raiola unaweza kuharibu uhamisho wake katika ligi ya Uingereza ,huku ikiaminika nchini Uholanzi kwamba klabu za Uingereza hazipendelei kufanya kazi na ajenti huyo.. Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal, Chelsea na Tottenham zote zinamlenga kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)
 
Winga wa Juventus winger Douglas Costa, 28, ametoa ishara kuhusu hatma yake ya siku zijazo alipopenda ujumbe wa twitter unaomuhusisha na uhamisho wa Manchester United. (Sun)
 
Manchester City imeharakisha usajili wa kipa Gavin Bazunu, unaomfanya kinda huyo mwenye umri wa 16 kuichezea timu yake ya wachezaji wake wasiozidi miaka 18 siku ya Jumamosi-. (Manchester Evening News)
 
Manchester United na Arsenal watatuma maskauti wao katika mechi ya Jumapili ya debi la East Anglian ili kumchunguza beki wa Norwich anayedaiwa kugharimu £10m Ben Godfrey, 21, ambaye amevutia klabu kama vile Lyon na RB Leipzig. (Mirror)
 
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Monchengladbach Max Eberl anatumai kwamba klabu hiyo itaweza kumshawishi Thorgan Hazard ambaye amehusishwaa na uhamisho wa Liverpool, kutia kandarasi mpya. (Inside Futbol)
 
Revolutionary leader.
Imam Khomein
FB_IMG_1549897616240.jpeg
 
Back
Top Bottom