Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tafsiri yake ni kwamba? Haturidhiki hata tupewe nini, hatuna aibu na tumekosa uaminifu kabisa. Kwamba mwanaume mpatie kila kitu anachostahili kupewa, mpe na vya ziada lakini linapokuja suala la kuwa mwaminifu na ndoa au uhusiano lazima atavuka mipaka tu, atatoka nje.
 
Tusikatae, yawezekana ikawa kweli, kwamba kuna wanaume si waaminifu, lakini mashaka yanakuja pale unapogundua mwanamke anayesema wanaume ‘wote’ ni mbuzi, hajawahi kuwa na uhusiano na hata nusu ya wanaume wa mtaa anaoishi – suala la wote linatokea wapi?
 
Wanawake wanakosea kuelewa, tatizo hapa halipo kwa wanaume, lipo kwenye asili ya binadamu. Roho zetu ziliumbwa na kitu kupenda, kupenda vitu vizuri. Kuna wakati binadamu anapopenda kitu kizuri anaweza kufanya chochote ilimradi apate, roho yake itulie.
 
Tafsiri yake ni kwamba, hapa tatizo linaweza lisianzie kwa mwanaume, likaanzia kwa wanawake wengine huko nje. Kwa sababu labda mwanaume ana kitu kizuri wanachopenda wanawake mathalani pesa. Unaweza kukuta wanawake wanaanza kutengeneza mazingira ya kukipata bila kujali hali ya uhusiano wa mwanaume, kwamba ameoa, ana mchumba au vipi. Hiyo kwake haimhusu, ishu ni ana pesa, anazitaka.
 
Kwa hiyo mwanaume anapokutana na majaribu mengi ya aina hii, kama imani yake ni ndogo, unakuta ni rahisi sana kufanya vitu vya ajabu.
 
Kumbe si wanaume wote wabaya, waaminifu tupo ila hamtuwazi kwa sababu tu hatuna fedha. Kama ambavyo kuna wanawake waaminifu ila hawaonekani kwa sababu hawana mawowowo.
 
Hii inaweza kuwa sawa na kwa wanawake; baadhi ya wanaume tunasema wanawake si waaminifu, lakini kimsingi inawezekana kuna wanawake waaminifu ni wengi sana, tatizo hawana mambo tunayoyapenda – mathalani mawowowo.
 
Kumbe si wanaume wote wabaya, waaminifu tupo ila hamtuwazi kwa sababu tu hatuna fedha. Kama ambavyo kuna wanawake waaminifu ila hawaonekani kwa sababu hawana mawowowo.
 
Baada ya kupiga kelele kwa muda mrefu kuhusu gharama za taulo za kike hadi Serikali kufikia hatua ya kuziondolea Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Upendo Peneza amegeukia suala la nguo za ndani.
 
Mbunge huyo wa viti maalum (Chadema), amesema gharama za nguo hizo, hasa maeneo ya vijijini, huwafanya mabinti kushindwa kununua na matokeo yake kuchangia hata taulo za kike zisitumike kwa usahihi.
 
Kufuatia hali hiyo Peneza alisema ipo haja kwa wizara ya fedha na mipango kuwa na dawati maalum la kijinsia litakalofanya kazi ya kuangalia masuala ya kijinsia na mwingiliano wake katika bajeti.

Kwa mujibu wa mbunge huyo uwepo wa dawati hilo utasaidia kuiwezesha Serikali kujua namna gani ya kusaidia upatikanaji wa bidhaa ambazo zinatumiwa na wanawake katika maisha yao ya kila siku.
 
Serikali ifanye utafiti kuangalia bidhaa muhimu kwa wanawake mfano nguo za ndani zinaweza kuingizwa kwa gharama gani hadi kumfikia mhusika wa kawaida na ikiwezekana kuwa na bei elekezi ya kawaida kabisa ambayo watu wa hali zote wanaweza kumudu,” alisema.

Pia alitoa wito kwa wazazi kuhamasika kujua mahitaji ya mtoto wa kike na kumtengea fungu lake kwa ajili ya kupata mahitaji hayo.
 
Kuhusu taulo za kike alisema pamoja na kuondolewa kwa VAT bado taulo hizo zinauzwa kwa gharama ya juu kutokana kuwepo kwa kodi nyingine.

“Nilishaongea na kamishna wa (Mamlaka ya Mapato Tanzania) TRA kuhusu taulo hizi kuendelea kuwa bei juu akaniambia atafanyia kazi.”

“Ningeshauri Serikali iondoe kodi zote zinazohusika na uzalishaji na uingizaji wa taulo hizi ili ziuzwe kwa gharama nafuu na upatikanaji wake uwe wa uhakika hasa mashuleni,” aliongeza.
 
Juzi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alieleza kuwa ameanza kuchukua hatua kwa kumuandikia barua waziri wa fedha na waziri wa viwanda kuhusu taulo hizo kuendelea kuuzwa kwa gharama kubwa.
 
Nimewaandikia waziri wa fedha na viwanda na biashara kuwataka waingizaji wa taulo za kike kupunguza bei ili kuhakikisha lengo la Serikali kuhakikisha wanawake wengi hasa wasichana walioko shuleni wanapata vifaa vya kujistiri kwa gharama nafuu, Sh2000 bado ni kubwa,”

Waziri huyo pia aligusia suala la ufungashaji wa taulo hizo kwa kile alichodai kuwepo na wafanyabiashara ambao wanazifunga kwa idadi ndogo ambayo haiwezi kukidhi mahitaji ya binti wakati wa hedhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…