Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.
 
Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.
 
Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.
 
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.
 
Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.
 
Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.
 
Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….
 
Inawezekana wewe ni moja kati ya ambao wamewahi kukosa usingizi wakati wa usiku. Hii huwa ni hali ambayo mara nyingi inasumbua na kukera hususani kama mtu umechoka.
 
1.Fanya mazoezi wakati wa mchana

Inashauriwa kuwa pindi ukigundua unapata wakati mgumu kulala wakati wa usiku mara kwa mara, tengeneza utaratibu wa kufanya mazoezi nyakati za mchana. Kwa kufanya hivi mwili na akili huandaliwa kwa ajili ya kupata usingizi wakati wa usiku.
 
2. Kuwa na muda binafsi na tafakari ilivyokuwa siku yako.

Kabla ya kulala pia inashauriwa kupata muda binafsi ili kutafakari yaliyotokea kwa siku hiyo na jinsi siku inayofuata inaweza kuwa nzuri na ya mafanikio. Katika hili inashauriwa kuacha kutumia simu au komputa pindi unapopanda kitandani badala yake funika macho na tafakari kuhusu siku hiyo, itakusaidia kulala.
 
4. Soma kidogo vitu chanya

Jambo jingine ni kutafuta kitu cha kusoma chenye ujumbe au taarifa za msingi na zilizo chanya. hatahivyo inashauriwa kisiwe kitu kirefu. Inaweza kuwa kitabu cha hadithi, jarida, makala na vinginevyo.
 
5. Kuwa na ratiba maalumu ya kulala

Hii ni pale ambapo unakuwa na muda maalumu wa kulala na kuamka kila siku bila kuivuruga. Suala hili litautengenezea mwili mazoea ya kupumzika kwa wakati fulani lakini pia litakusaidia kuamka bila uchovu au maumivu yoyote ya mwili. Hii pia itasaidia kulala bila shida kwa wakati uliozoea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…