Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6. Chunga tabia yako ya kulala

Ni muhimu sana kuzingatia kuachana na vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la kushindwa kulala wakati wa usiku ikiwa ni pamoja na kulala wakati wa jioni jambo linaloweza kukata usingizi pindi muda wa kulala unapofika wakati wa usiku.
 
7. Acha kuangalia TV nyakati za usiku sana

Pia ni muhimu kuachana na tabia ya kukaa macho na kuangalia TV nyakati za usiku mwingi kwani mwili hujijengea kutolala wakati huo unapofika kwani huwa ni muda ambao kwa kawaida unakuwa unaangalia TV.

Pia mwanga wa TV unaelezwa kukandamiza homoni ya melatonin inayosaidia mwili wa binadamu kulala au kuamka pindi muda muafaka unapofika.
 
8. Chunga unachokula au kunywa kabla ya kulala

wataalamu pia wanashauri kuwa ni muhimu kuangalia vitu vya kula au kunywa unapoelekea muda wako wa kulala. Inashauriwa kuepuka kunywa kahawa au pombe kabla ya kwenda kulala kwa sababu ni vitu ambavyo vinachukua muda mrefu kuyeyushwa tumboni.
 
9. Andaa mazingira mazuri ya kulala

Kulala kwenye mazingira mazuri ni muhimu. Inashauriwa kulalia mashuka masafi na mito misafi, huku eneo zima kama chumbani liwe safi lisilo na vumbi wala harufu.

Pia kama huwezi kulala kukiwa na muziki usiwashe muziki lakini pia kama kukiwa muziki unapata usingizi mzuri basi unashauriwa kufanya hivyo.
 
10. Tumia choo kabla hujalala

Baadhi ya watu hupoteza kabisa usingizi na kushindwa kuupata tena pindi wanapoamka usiku ili kwenda chooni au kwa sababu nyingine zozote. Kwa mantiki hiyo wataalamu wanashauri ni vyema kwenda haja kabla ya kwenda kulala ili kwamba mwili usisumbuliwe wakati umelala.
 
IMG_4471.JPG

Mwanamke dimples bana! [emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550]
 
Back
Top Bottom