Klopp ataingia kwenye mechi hiyo ya leo huko Anfield akiwa hana huduma ya mabeki wake, Dejan Lovren, Joe Gomez na Virgil van Dijk kutokana na kuwa majeruhi na wengine kutumikia adhabu, hivyo kumfanya awe na chaguo la kumtumia Fabinho na Joel Matip kwenye beki ya kati. Silaha pekee anayotarajia kuitumia Klopp ni kuwapa kazi washambuliaji wake, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane kuhakikisha wanawashambulia Bayern Munich.