Wachezaji wa Barcelona walionekana kuwa na presha zaidi baada ya kupata suluhu ya bila kufungana mchezo uliopigwa Uwanja wa Groupama jana Jumanne usiku.
Baada ya dakika 90 kumaliza nyuso za wachezaji wa Barcelona iliashiria kuumizwa na suluhu hiyo. Hiyo ni kutokana na nafasi nyingi ambazo wachezaji walizipata langoni kwa Lyon takribani 25 lakini walishindwa kufunga mabao.
Kwenye mchezo huo mwamuzi Cuneyt Cakir aliwazawadia kadi za njano wachezaji wa Lyon Housem Aouar na Leo Dubosi, huku wachezaji wa Barcelona, Nelson Semedo na Sergi Roberto nao walilimwa kadi za njano.
Matokeo ya bila kufungana jana Jumanne usiku mchezo wa hatua ya 16 Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Liverpool na Bayern Munich yameacha simanzi kwa Kocha Jurgen Klopp.
Bayern Munich ambao walikuwa ugenini walionekana kuwavuruga Liverpool tangu kipindi cha kwanza kwenye dimba la Anfield kutokana na kuwa na safu imara ya ulinzi.
Alisema kipindi cha kwanza walipata nafasi nyingi ambazo walizitengeneza lakini hali ikawa tofauti kipindi cha pili na hakuna aliyekuwa akihangaika kutengeneza nafasi.
Kocha wa Bayern Munich, Noko Kovac alisema baada ya kupata suluhu kwenye mchezo wake dhidi ya Liverpool anaangalia nini cha kufanya kuhakikisha mchezo unaofuata wanafanya vyema zaidi.