Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zifuatazo zinaweza kuwa kadi nyekundu za kipuuzi zaidi ambazo Ramos amewahi kupewa.

Ramos vs Girona – 2019

Kadi ambayo ameipata karibuni zaidi. Baada ya kikosi cha Real Madrid kuanza kurudi katika fomu kufuatia mwanzo wao mbovu msimu huu, Ramos aliiangusha timu yake katika pambano hili dhidi ya Girona. Madrid ilikuwa imechapwa bao 1-0. Ramos akaunawa mpira kijinga na kuipa Girona penalti ambayo walifunga bao la kusawazisha. Baadae kidogo Girona wakafunga bao la pili. Kuanzia hapo Ramos akataka kuongoza kwa vitendo kutafuta bao la kusawazisha. Katika harakati hizo akajikuta anapiga tiktak na kuukosa mpira huku kiatu chake kikitua katika sura ya mchezaji mmoja wa Girona. Akalambwa kadi ya pili ya njano kisha nyekundu.
 
Ramos vs Ajax – 2010

Hapa nahodha alifanya kitu cha kijinga cha kushangaza. Wakati timu yake ikiongoza mabao 4-0 ugenini dhidi ya Ajax pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Ramos aliamua kujipa kadi ya pili ya njano kijinga kwa kuchelewesha mpira kwa makusudi ili apewe kadi nyekundu na kisha alikose pambano la marudiano kwa ajili ya kusafisha kadi zake na aende robo bila ya kadi.
 
Alipewa kadi ya pili na kisha nyekundu na badala ya hapo Ramos hakuwa yule ambaye tunamfahamu. Hakukasirika na badala yake alimpa mkono mwamuzi na kumuaga huku akienda zake nje. Hivi karibuni amerudia tena ujinga wake katika pambano kama hilo dhidi ya Ajax Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Amejipa kadi ya njano za makusudi ili akose pambano la marudiano Santiago Bernabeu na kuna uwezekano akafungiwa zaidi ya mechi moja kutokana na kugundulika kufanya jambo hilo kwa makusudi.
 
Ramos vs Barcelona – 2010

Kadi yake ya kwanza miongoni mwa kadi tano nyekundu ambazo amejikusanyia El Clasico mpaka sasa. Ilianzia katika rafu ambayo Lionel Messi alichezewa na wachezaji wa tatu wa Real Madrid kwa mpigo. Likazuka zogo kubwa na Ramos akajichukulia kadi yake kiulaini baada ya kumsukuma wazi wazi mlinzi mwenzake mkongwe wa Hispania. Carles Puyol usoni huku akianguka chini kama gunia. Hata wenzake walimshangaa. Wakati anatoka nje akaendeleza utukutu kwa kumsukuma kwa kidole cha usoni, Xavi Hernandez. Hapana shaka ukweli ni kwamba hasira zake zilitokana na Barcelona kuongoza 5-0 mpaka wakati huo.
 
Ramos vs Villarreal – 2012

Ilikuwa ni siku ya kuvunja rekodi kwa Sergio Ramos. Ilikuwa ni siku ambayo alikuwa anaichezea Real Madrid mechi ya 300 lakini hakutuacha hivi hivi. Siku hiyo hiyo akavunja rekodi ya kuonyeshwa kadi nyekundu nyingi katika historia ya La Liga. Pambano lilitawaliwa na ugomvi mwingi na Ramos alionekana akimpiga teke kisha kiwiko mshambuliaji wa Villarreal, Nilmar. Hasira zilitawaliwa pambano hilo kiasi kwamba Mesut Ozil naye alitolewa nje kwa kadi nyekundu huku kocha Jose Mourinho pia akipelekwa jukwaani. Pambano lilimalizika kwa sare ya 1-1.
 
Ramos vs Celta Vigo – 2013

Katika pambano hili Ramos alifanya ujinga mwingine usio na maana kama kawaida. Alimkanyaga kifuani kiungo wa Celta Vigo, Augusto Fernandez huku akijifanya kama vile hakukusudia na kuwahi kumuomba msamaha. Alifungiwa mechi tano huku pia adhabu hiyo ikitokana na kumshambulia mwamuzi baada ya mechi hiyo akidai alikuwa ni ‘fedhea’ kwa upande wa Madrid.
 
Ramos vs Rayo Vallecano – 2013

Ilikuwa mechi ya kushangaza sana kwa Ramos. Ndani ya dakika 18 za mwanzo alikuwa ameshaifungia Real Madrid mabao mwili na kuifanya iongoze kwa mabao 2-0. Lakini ndani ya dakika hizo hizo alikusanya kadi mbili za njano ndani ya dakika moja na kujikuta akielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo. Kadi ya pili ya njano bado inadaiwa kuwa na utata kama alikuwa ameshika mpira au vinginevyo.
 
Ramos vs Malaga – 2008

Kadi nyingine ya kipuuzi kwa Ramos. Katika mechi hii iliyokuwa na upinzani mkali Ramos aliamua kumkanyaga kifuani mlinzi wa kushoto wa Malaga, Eliseu aliyekuwa amelala chini bila ya hatia. Alijifanya kuomba msamaha haraka haraka kwa Eliseu lakini mwamuzi alikuwa amekwishamuona. Pambano lilikwenda sare ya 2-2 hadi mapumziko huku Ramos akiwa ameshaoga na kubadili mavazi yake.
 
Ramos vs Barcelona – 2017

Katika kadi tano alizopewa mechi za El Clasico hapa tumeamua kuweka mechi mbili tu mpaka sasa ingawa nyingine inakuja. Hii ni mechi nyingi ambayo alipewa kadi nyekundu kwa kumrukia Lionel Messi miguu miwili huku zikiwa zimebakia dakika 13 mechi kumalizika Barcelona wakiongoza 2-1. Wakati akipewa kadi hiyo aliamua kumsukuma kidogo mwamuzi. Messi akawafungia Barcelona la ushindi katika dakika za zilizobaki huku matokeo hayo nusura yaligharimu Madrid ubingwa.
 
Ramos vs Barcelona – 2016

Akiwa amerudi kutoka katika adhabu ya kufungiwa Ramos hakuonekana kama anajali sana hilo. Hapa alimrukia vibaya Luis Suarez na kupewa kadi nyekundu moja kwa moja iliyompeleka katika vyumba vya kubadilishia nguo. Wakati huo pambano lilikuwa sare ya 1-1. Wakiwa pungufu Cristiano Ronaldo aliamua kufuta ujinga wa Ramos kwa kufunga bao la ushindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…