Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini uhamisho huo haukufanikiwa hivyo kufanya kikosi cha wachezaji 22 cha Klopp kuwa na wachezaji saba kutoka England, watatu (Brazil), wawili (Uholanzi) huku Ubelgiji, Cameroon, Croatia, Misri, Guinea, Ureno, Senegal, Hispania, Uswisi na Scotland kila moja ikitoa mchezaji mmoja.
 
Kutokana na mazingira hayo Manchester City iliyotumia pauni 54milioni kumnunua beki Mfaransa Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao mwaka 2018 – kuwa na tumaini la kutwaa ubingwa? Historia inaonyesha unahitaji kuwa Mfaransa hivyo City wapo vizuri kwa sababu pia wanaye Benjamin Mendy.
 
Fergie amekuwa na mapenzi na Wafaransa akianzia katika enzi za Eric Cantona. Pia, alimsajili kipa Fabien Barthez katika mwaka 2000 na kufanikiwa kutwaa mataji mwaka 2001 na 2003.
 
Wakati Ferguson akijenga upya kikosi chake, alimnunua beki wa kushoto Patrice Evra aliyekuwa na mchango mkubwa kwa Man United na kufanikiwa kutwaa mataji mwaka 2007, 2008, 2009, 2011 na 2013.
 
WAFARANSA WALITWAA UBINGWA WA LIGI KUU

Eric Cantona (Manchester United) - 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97

Nicolas Anelka (Arsenal) - 1997-98, 2009-10

Remi Garde (Arsenal) - 1997-98

Gilles Grimandi (Arsenal) - 1997-98, 2001-02
 
Emmanuel Petit (Arsenal) - 1997-98

Patrick Vieira (Arsenal) - 1997-98, 2001-02, 2003-04

Mikael Silvestre (Manchester United) - 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07

Fabien Barthez (Manchester United) - 2000-01, 2002-03

Thierry Henry (Arsenal) - 2001-02, 2003-04
 
Robert Pires (Arsenal) - 2001-02, 2003-04

Sylvain Wiltord (Arsenal) - 2001-02, 2003-04

Laurent Blanc (Manchester United) - 2002-03

Jeremie Aliadiere (Arsenal) - 2003-04

Pascal Cygan (Arsenal) - 2003-04

Gael Clichy (Arsenal, Manchester City) - 2003-04, 2011-12, 2013-14
 
William Gallas (Chelsea) - 2004-05, 2005-06

Claude Makelele (Chelsea) - 2004-05, 2005-06

Patrice Evra (Manchester United) - 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13

Louis Saha (Manchester United) - 2006-07, 2007-08
 
Ubingwa wa kwanza katika Karne hii, Manchester United ilitwaa ikiwa na Mikael Silvestre hakuna mchezaji aliyeanza mechi nyingi zaidi yake katika msimu wa 1999/2000 chini Sir Alex Ferguson.
Umetoa ile avatar ya katoto innocent kenye dimples na kurudisha hii ya kishari shari eeh!? Hii angalau kidogo inakurudishia u rolo modo kidogo. Kale katoto ulikuwa unakaonea tu kwa kweli kwa sababu hamuendani kabisa [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…