Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Liverpool na Manchester City walikuwa wakitazamana kijicho kuelekea mechi zao hizo huku kila mmoja akimuombea mabaya mwenzake lakini wote walishinda katika mechi zao za nyumbani na tofauti imeendelea kubakia pointi moja baina yao.
 
Liverpool ilimchapa Watford mabao 5-0 Anfield huku City ikiondoka kwa ushindi mwembamba nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya West Ham na Liverpool imeendelea kuongoza ligi kwa pointi 69 wakati City inapumua nyuma yake kwa pointi 68. Inavyoelekea mpambano utakwenda mpaka Mei.
 
Arsenal ilishinda mechi yake dhidi ya Bournemouth mabao 5-1 na inashika nafasi ya nne akiwa na pointi 56 lakini nyuma yake kuna Manchester United ambayo ilishinda ugenini dhidi ya Crystal Palace ikiwa na wachezaji wengi majeruhi nje ya uwanja na inasimama nafasi ya tano ikiwa na pointi 55.
 
Nyuma yao kuna Chelsea yenye pointi 53 lakini ina mechi moja mkononi baada ya pambano lao dhidi ya Everton kuahirishwa wikiendi iliyopita ambapo ililazimika kucheza na Manchester City katika fainali za Kombe la Ligi.
 
Lolote linaweza kutokea mpaka mwishoni mwa msimu lakini kuna mechi kubwa ambazo zitakutanisha vigogo wenyewe kwa wenyewe na kwa kiasi kikubwa zitaamua hatima yao kuelekea mwishoni mwa msimu huu Mei 12.
 
Kwa kuanzia kesho Jumamosi mchana kutakuwa na pambano kati ya Tottenham dhidi ya Arsenal katika dimba la Wembley. Pambano hili kwa kiasi kikubwa litaashiria nguvu za Arsenal katika kubaki Top Four pamoja na kuitishia Tottenham katika nafasi ya tatu.
 
Endapo Arsenal itashinda mechi hii itabakiza pointi moja tu nyuma ya Tottenham na kutishia kuichukua nafasi ya tatu baada ya Spurs kuteleza katika mechi za karibu ikipoteza kwa vipigo kutoka kwa Burnley na Chelsea.
 
kwanza kabisa, Tottenham inaweza kutumia nafasi hiyo katika kujirudisha katika mbio za ubingwa huku pia wakijiimarisha katika mbio za Top Four kama ikiharibikiwa zaidi katika mechi zao kabla ya hapo ikiwemo pambano dhidi ya Arsenal kesho. Lakini Liverpool inaweza kukwama katika mbio za ubingwa kama wakitibuliwa.
 
April 14 kuna pambano kati ya Liverpool na Chelsea ambalo nalo ni fainali ndogo ambayo itaamua mbio za ubingwa kwa Liverpool na zile za Top four kwa Chelsea ambayo msimu huu imeonekana kuwa nyanya katika mechi dhidi ya wakubwa wenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…