Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa upande wa watu wenye matatizo ya presha ya kushuka, mara nyingi vinywaji hivi vimekuwa ni msaada mkubwa kwao. Kwani vinaongeza nguvu ya moyo katika kusukuma damu na hatimaye kuifanya presha iongezeke.
 
Kutokana na kafein kuweza kuifanya presha ipande, mara kadhaa imekuwa ikisababisha changamoto katika kupima presha na pia kuandika dozi ya dawa pindi mgonjwa anapokuwa ametumia vinywaji vyenye mchanganyiko huo.
 
Kafein huweza kuifanya presha ipande kwa masaa matatu mara baada ya kuitumia, kwa kufanya hivyo na endapo hapatakuwa na taarifa za matumizi hayo basi huweza kupelekea kwa mtu ambaye hana presha ya kupanda aonekane kama ni mwenye tatizo hilo wakati wa kufanyiwa vipimo. Pia huweza kusababisha mgonjwa akaandikiwa dozi kubwa ya dawa za presha tofauti na uhalisia.
 
Dawa zinazotumika kutibu presha ya kupanda, kwa namna moja ama nyingine ufanyajikazi wake unakinzana na kafein. Sababu za presha kupanda moja wapo ni moyo kusukuma damu kwa haraka, kafein pia huufanya moyo usukume damu kwa haraka.
 
Miongoni mwa dawa ambazo ufanyaji kazi wake unakinzana na kafein ni pamoja na Propranolol na Metoprolol ambazo ufanyaji kazi wake unakuwa hafifu pindi mtumiaji wa dawa hizo atazitumia sambamba na kafein.
 
Ili kuweza kuulinda moyo wako na pia kuziwezesha dawa za presha ziweze kufanya kazi ipasavyo, ni vyema kuchukua tahadhari katika matumizi ya kafein kwani ni moja ya vitu vinavyoweza kuifanya presha yako ipande.
 
Kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa watumiaji wa mara kwa mara wa vinywaji vyenye kafein, inafika wakati wakikosa kutumia wanapatwa na maudhi madogo madogo mfano kujisikia kichwa kinauma ama kujisikia kama mwili hauko sawa.
 
Hii hutokea kutokana na moja ya sifa za chembechembe hii, kafein (caffeine), kwa namna moja ama nyingine huufanya mwili kuwa na hali ya kuizoea na kuihitaji, ambapo kwa kitaalamu hujulikana kama caffeine addiction.
 
Back
Top Bottom