Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

455020619_145587.jpeg
 
Ni timu tatu tu-- Barcelona, Roma na Deportivo La Coruna -- zimefanikiwa kugeuza matokeo ya kipigo cha mabao matatu kwa kufunga idadi kama hiyo ya mabao au zaidi katika hatua ya mtoano katika enzi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
 
Barcelona yaishangaza PSG
hatua ya 16 bora msimu wa 2016/17
Mechi ya kwanza: Paris Saint-Germain 4 Barcelona o
(Mabao: Di Maria 18, 55 Draxler 40, Cavani 72)
Mechi ya marudiano: Barcelona 6 PSG 1
Mabao (Suarez 3, Kurzawa 40-kujifunga, Messi 50-penati, Neymar 88, 90+1-penati, Roberto 90+5); Paris Saint-Germain (Cavani 62)
Barcelona ilisonga mbele kwa jumla ya mabao 6-5
 
Barcelona iliweka historia ya kuwa timu ya kwanza ambayo iliruhusu mabao manne katika mechi ya kwanza lakini ikashinda mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Nou Camp na kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika mechi ambayo Neimar aliiadhibu kwa kufunga mabao mawili timu ambayo baadaye alijiunga nayo.
 
Kama kipigo cha PSG mbele ya kikosi cha Luis Enrique jijini Paris kilikuwa cha kustua, ushindi katika mechi ya marudiano uliotokana na mabao mawili yaliyofungwa katika muda wa nyongeza, ulikuwa wa kufikirisha.
Sergi Roberto alitokea benchi na kujiandikia historia katika soka nchini Hispania alipofunga bao la sita katika muda wa nyongeza.
"Sikujua kama nilikuwa naota –- sijawahi kusikia sauti za kelele kama hizi," alisema Roberto baada ya filimbi ya mwisho.
 
Bahati ya Barca yapotea jijini Rome
Robo fainali, 2017/18
Mechi ya kwanza: Barcelona 4 Roma 1
(Mabao: De Rossi 38-la kujifunga, Manolas 55-la kujifunga, Pique 59, Suarez 87; Dzeko 80)
Mechi ya marudiano: Roma 3 Barcelona 0
(Mabao: Dzeko 6, De Rossi 58-penati, Manolas 82)
Roma ilisonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini.
Bahati ya Barcelona ilipotea kwa njia ya kipekee katika kipindi cha miezi 12 baada ya kuiondoa PSG baada ya Edin Dzeko kufunga bao muhimu la ugenini kwenye uwanja wa Nou Camp.
 
Mshambuliaji huyo raia wa Bosnia alipata shida kueleza furaha yake kutokana na mafanikio ya Roma baada ya bao lake alilofunga katika dakika ya sita katika mechi ya marudiano kufungua mlango wa wataliano kuzindika katika hatua hiyo.
 
Hata hivyo, baada ya bao la Dzeko alilofunga mwanzoni, bao la penati lililofungwa na Daniele De Rossi lilifungua njia kwa Kostas Manolas kufunga bao la kichwa katika dakika ya 82 liliamsha shangwe zilizoongozwa na rais wa Roma, James Pallotta, ambaye kuonyesha furaha yake alikwenda kurukia kwenye bwawa la maji katika bustani ya Piazza del Popolo jijini Rome.
 
Miujiza ya Irureta
Robo fainali, 2003/04
Mechi ya kwanza: AC Milan 4 Deportivo La Coruna 1
(Mabao: Kaka 45, 49, Shevchenko 46, Pirlo 53; Pandiani 11)
Mechi ya marudiano: Deportivo La Coruna 4 AC Milan 0
(Mabao: Pandiani 5, Valeron 35, Luque 44, Fran 76)
Deportivo ilisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4.
Baada ya timu yake kubamizwa kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa San Siro, kocha wa Deportivo, Javier Irureta alikiri kuwa hakukuwa na sababu ya kuamini katika miujiza.
Hata hivyo, timu yake ilimudu kufanya kile alichokuwa haamini baada ya kufunga na kuongoza kwa mabao 3-0 kabla ya mapumziko, wafungaji wakiwa ni Walter Pandiani, Juan Carlos Valeron and Albert Luque.
 
Fran Gonzalez, aliyeanzia benchi, aliongeza bao la nne zikiwa zimesalia dakika 14 mchezo kumalizika na akiwa ameomba apate mafanikio, Irureta alitimiza ahadi yake aliyotoa kabla ya mechi ya kwenda Santiago de Compostela baada ya ushindi huo ambao haukutarajiwa.
 
Mario Balotelli jana Jumapili alionyesha aina mpya ya ushangiliaji wa bao wakati alijipiga picha uwanjani akiwa na wachezaji wenzake na kuituma kwenye mtandao wa kijamii.
Mtaliano huyo alifunga bao lake la nne katika mechi sita alizocheza tangu ajiunge na Marseille klabu ya Nice Januari. Aliunganisha kwa tik-tak kona iliyopigwa na Florian Thauvin katika dakika ya 12.
 
Back
Top Bottom