Miujiza ya Irureta
Robo fainali, 2003/04
Mechi ya kwanza: AC Milan 4 Deportivo La Coruna 1
(Mabao: Kaka 45, 49, Shevchenko 46, Pirlo 53; Pandiani 11)
Mechi ya marudiano: Deportivo La Coruna 4 AC Milan 0
(Mabao: Pandiani 5, Valeron 35, Luque 44, Fran 76)
Deportivo ilisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4.
Baada ya timu yake kubamizwa kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa San Siro, kocha wa Deportivo, Javier Irureta alikiri kuwa hakukuwa na sababu ya kuamini katika miujiza.
Hata hivyo, timu yake ilimudu kufanya kile alichokuwa haamini baada ya kufunga na kuongoza kwa mabao 3-0 kabla ya mapumziko, wafungaji wakiwa ni Walter Pandiani, Juan Carlos Valeron and Albert Luque.