Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huenda Isco angepatikana kirahisi tu kama kusingekuwa na timu nyingine zinazomkimbiza, lakini upatikanaji wa mchezaji huyo unazidi kuwa mtihani kutokana na klabu kibao kumtolea macho ikiwemo Liverpool.
 
kikosi cha Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp kilitoka suluhu na everton, na jambo hilo limewafanya washuke kwa pointi moja (70) katika mbizo za ubingwa wa Ligi Kuu Engand dhidi ya Manchester City (71). Lakini Klopp ameibuka na kutoa lawama kwa hali ya hewa akidai ndio ilisabisha suala hilo.
 
Klopp anafahamu sasa anatakiwa kuwa makini zaidi katika mbio za ubingwa kwa kuwa zimebaki mechi nane tu kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2018/19. Wapenzi wa Liverpool walikuwa na mshituko baada ya mechi hiyo lakini Klopp alikuwa na haya ya kujitetea.
 
Ilikuwa ni mechi ambayo ni ngumu kuidhibiti. Tulikuwa na nafasi mbili au tatu lakini hazikuweza kupata matunda. Tumetoka suluhu, kwa hiyo tumeendelea kuwa na rekodi ya kutokuchapwa kwa mechi kadhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…