Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika kukisafisha kinywa, kila mtu anafahamu namna anavyokisafisha kinywa chake, mambo anayoyafanya kabla na baada ya kutumia mswaki wake na pia utunzaji wa mswaki wake. Katika mswaki na kinywa, leo kunabaadhi ya mambo ambayo ninapenda tukumbushane.
 
Katika mwili wa binadamu, hii ni pamoja na katika vinywa vyetu, siku zote huwa na wadudu (bacterias) maelfu kwa maelfu wa aina mbali mbali, wapo wadudu wanaosababisha magonjwa na pia wale ambao ni salama katika miili yetu, kadharika na katika mazingira yetu, katika hewa na vingine vyote vinavyotuzunguza pia huwa na wadudu mbalimbali.
 
Pamoja na kuwepo wadudu hawa katika mazingira na pia katika miili yetu, mtu atapata magonjwa endapo uwiano kati wa wadudu wanaosababisha magonjwa na wadudu ambao ni salama utabadilika kwa maana ya mwili ukiwa na wadudu wengi wanaosababisha magonjwa na pia endapo kinga yake ya mwili (Immunity) yake ikishuka, ndipo atakapopata ugonjwa.
 
Tafiti zinaonyesha kuwa, mswaki ulioachwa wazi, hubeba mamia kwa mamia ya wadudu (bacterias) wakiwemo wale wasababishao kuharisha, E. Coli, wasababishao magonjwa ya ngozi, Staphylococci na wengine wengi.
 
Hii inamaana kwamba, kila unapotumia mswaki kuna aina fulani ya wadudu (bacterias) unaowaweka katika kinywa chako, pia kuna wadudu unaowarudisha katika kinywa chako kwani kama tulivyoona hapo awali kuwa, katika mwili (kinywa) siku zote wadudu wapo.
 
Hivyo unapoutumia mswaki kuna wadudu unaowatoa na kuwaweka katika mswaki, unapokuja kuutumia mswaki wako tena unawarudisha wale ambao tayari ulikuwa unao.
 
Hii ni sababu mojawapo inayochangia kuwepo kwa magonjwa ya kujirudiarudia ya kinywa/meno. Ila mwili siku zote unayo kinga na uwezo wa kujilinda, ugonjwa utatokea endapo kinga yako itashuka au endapo mswaki mmoja utatumiwa na mtu zaidi ya mmoja.
 
Wewe ndiye unayefahamu mswaki wako unauhifadhi wapi, tafiti zinaonyesha kuwa chombo cha kuhifadhia mswaki (Toothbrush Holders) kinashika nafasi ya tatu kwa uchafu ndani ya nyumba, hii inatokana na kutopewa umakini wa kutosha pindi usafi unapofanyika nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…