Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3.Mabadiliko ya mchezaji

Tofauti na zamani mabadiliko ya mchezaji yalikuwa yakifanyikia kwa mwamuzi wa akiba, kuanzia muda ambao kanuni hizo mpya zitaanza kutumika, mchezaji anayefanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja.
 
.
FB_IMG_1549216871699.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
7. Pigo la penati

Makipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi, tofauti na sasa miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati. Mabadiliko hayo yamepelekea maoni na mitazamo tofauti kwa wadau wa mpira wa miguu nchini ambao hata hivyo wameyapongeza.
 
Phillip Alando- Meneja Azam

“Ni jambo zuri na nadhani IFAB na Fifa wameangalia mbali na wana nia njema na ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu. Kwa mtazamo wangu kanuni zilizonifurahisha zaidi ni hiyo ya kadi kwa makocha na maofisa wa benchi la ufundi kwa sababu itasaidia kuwapa nguvu makocha kufanya kazi kwa uhuru kwa sababu kanuni ya zamani imekuwa ikiziumiza timu.
 
Athuman Kazi - Mwamuzi Mstaafu

“Mara kwa mara mabadiliko haya yanapofanyika yanalenga kufanya watu wawe makini zaidi katika utafutaji wa mabao. Mfano utaratibu wa kumalizia penati inayookolewa na kipa au kugonga mwamba ulikuwa unapunguza umakini wa mpigaji na kumuonea kipa lakini kwa sasa wapigaji penati watakuwa na umakini wa hali ya juu kwa sababu wanajua wakikosa hakuna kumalizia.
 
Ally Mayay-Mchambuzi

“Mabadiliko yana mantiki na yataleta tija kwenye mpira wa miguu kwa mfano, kipengele cha kuzuia mchezaji wa timu inayopiga faulo kwenda kujipanga kwenye ukuta wa timu inayopigiwa, itaondoa vurugu ambazo hutokea mara kwa mara baina ya wachezaji ambao wamejipanga kwenye ukuta na yule wa timu inayopiga,” alisema Mayay.
 
Back
Top Bottom