Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbali na vita hiyo ya ubingwa, pia kuna vita kubwa ya kuwania nafasi kwenye ‘Top four’. Tottenham (pointi 61), Manchester United (pointi 58), Arsenal (pointi 57) na Chelsea (pointi 56), zinatoana jasho balaa. Tumeshashuhudia matukio ya kushangaza.
 
Tukiwa tumebakisha robo ya safari na inavyoonekana mpaka sasa ni ngumu kutabiri nani atabeba ubingwa wa EPL. Ukiachana na vita kubwa ilioko England na Ujerumani, huko Hispania, Ufaransa na Italia, ni kama shughuli imeisha.
 
Huko Ujerumani Bayern na Dortmund, zinashikana mashati. Ni vurugu tupu! Kama hiyo haitoshi, kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, nako mambo yameiva. Moto unawaka katika hatua ya 16 bora. Hata hivyo, hali hii inaweza kuathiri kampeni ya baadhi ya klabu, hapa tunatupia macho klabu tatu.
 
3. BORUSSIA DORTMUND

Borussia Dortmund, wenyewe walianza msimu kwa kasi kubwa na kuwaaminisha mashabiki wa Bundesliga kwa hakika msimu huu Bayern Munich, hawana chao.
 
Walionekana kupata fomu na kurudisha makali yao ya zamani. Waliwaaminisha wengi wamefanikiwa kutengeneza muunganiko mzuri wa kisoka kutokana na falsafa za soka la taifa la wajukuu wa Adolf Hitler; Ubabe na kipaji.
 
Ikiwa na wachezaji wenye vipaji halisi vya soka kama Jadon Sancho, Dan-Axel Zagadou, Achraf Hakimi na Manuel Akanji, kwa ushirikiano na wazee wa kutibua, Axel Witsel, Lukasz Piszczek, Mario Gotze na Marco Reus, ilikuwa ni ngumu kuamini Dortmund wangepata tabu kama wanavyopata hivi sasa.
 
Aidha, uchawi wa Kocha Lucien Favre unaonekana kumwingia Paco Alcacer vizuri. Dawa za Favre, zimeamsha mashetani yote yaliyolala katika mwili wa Mswisi yule, kuanzia kwenye akili hadi miguu. Yuko fiti kalikiti msimu huu.
 
Hata hivyo, kutokana na presha ya kushinda, ambayo ni kawaida kutokea ligi inapokaribia kufika ukingoni, Dortmund hii iliyojaza chipukizi kibao, inaonekana kuanza kukata pumzi. Kasi yao na ubabe wao umepungua.
 
Ile beki yao ambayo ilionekana kujengwa na ukuta imara hivi sasa imejaa nyufa kibao. Safu ya kiungo iliyotajwa kuwa bora kiasi cha kufananishwa na kiungo ya kina Xavi na Iniesta kule Barcelona, sasa hivi haipo tena. Safu yao ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inanyanyasa beki pinzani ilishajifia siku nyingi.
 
Mambo ni magumu na kinachowaweka kileleni ni wingi wa mabao tu. Wana pointi sawa na Bayern Munich inayoshika nafasi ya pili. Zote zna pointi 56. Bayern, ambayo iko vizuri, ina mabao 29, yaani tofauti kati yao ni pointi tatu tu.
 
2. REAL MADRID

Los Blancos, walianza msimu wa 2018/19 vibaya sana. Kasi waliyoanza nayo athari yake imeonekana katika kipigo cha 5-1 na 1-0 kwenye El Clasico. Majanga yalianza kwa kufutwa kazi kwa Julen Lopetegui. mrithi wake, Santi Solari amejitahidi kurudisha heshima Santiago Bernabeu lakini hali bado haijawa shwari kama zamani.
 
Mwezi februari, walitupwa nje kwenye Copa Del Rey na wapinzani wao Barcelona. Mbaya zaidi matumaini yao La Liga yanaonekana kufifia kadri siku zinavyozidi kwenda. Wako katika nafasi ya tatu kwenye msimamo, wakiwa na pointi 48, pointi 12 nyuma ya vinara Barcelona.
 
Hata hivyo, kitu pekee ambacho kinaendelea kuwapa kiburi ni ubabe wao kwenye Ligi ya Mabingwa ambayo wanatazamia kuchukua kwa mara ya nne mtawalia. wataweza kweli? tusubiri tuone.
 
Tangu Cristiano Ronaldo aondoke, Real Madrid imejikuta ikihangaika sana kupata mabao. pamoja na kuwa na kiwango kizuri katika siku za hivi karibuni, uhaba wa mabao katika viunga vya Bernabeu ni suala la kufanyiwa kazi, vinginevyo watakula kwa macho msimu huu.
 
Tofauti na miaka ya nyuma, beki ya Real Madrid imeonekana kukosa uimara. Marcelo ni kama bado anamuwaza swahiba wake Ronaldo na kuna uvumi huenda akahamia Italia msimu ujao. Luka Modric ametamka wazi hakuna wa kuziba pengo la Ronaldo huku, Sergio Ramos, siku hizi amekuwa bondia na sio beki.
 
1. LIVERPOOL

Liverpool walianza msimu vizuri. kasi yao ilikuwa inatisha balaa. Hadi kufikia mwezi Desemba walikuwa kileleni, pointi saba mbele ya mabingwa watetezi Manchester City. Mwanzoni mwa msimu, ilikuwa ni ngumu kuingia Anfield, ukatoka salama.
 
Beki yao, chini ya uongozi wa Virgil van Dijk, ilikuwa imara sana. Ilikuwa ni ngumu kupita, lakini kuanzia Mohammed Salah, Sadio Mane na Robert Firmino walipoanza likizo ya kufunga mabao, safu ya king ilipoanza kulala, kuanzia Virgil Van Dijk, alipoanza kuwa mpole, Liverpool ilipoteza uelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…