Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Rais wa Real Florentino Perez anaangalia uwezekano wa kumfuta kazi meneja Santiago Solari mara moja baada ya timu hiyo ya Ligi ya Championi kufungwa na Ajax Jumanne, lakini anahisi kwamba hakuna uwezo wa kuongoza kwa kipindi kilichobaki cha msimu. (Marca)
 
Everton haina mipango ya kumuuza mchezaji wa kiungo cha kati safu ya nyuma Mason Holgate msimu huu licha ya kuwa na nia ya kumnunua iliyoonyeshwa na timu ya West Brom, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anacheza kwa deni. (Liverpool Echo)
 
Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Newcastle Muhispania Ayoze Perez, mwenye umri wa miaka 25, anasema klabu hiyo inapaswa kurefusha mkataba wa meneja Rafael Benitez , huku mazungumzo ya mkataba huo yakiwa yamesimamishwa hadi itakapoweza kuingia katika Ligi kuu ya Uingereza. (Chronicle)
 
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amethibitisha kuwa klabu yake inamtaka mchezaji wa kati safu ya nyuma w Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, baada ya kusiani mkataba na mchezaji mwenzake kwenye timu hiyo Frenkie de Jong, mwenye umri wa miaka 21. (SER, via Independent)
 
Juventus wanaangalia uwezekano wa kuwaweka pamoja meneja wa zamani Antonio Conte na mchezaji wa zamani wa safu ya kati Andrea Pirlo kama msaidizi wake ikiwa meneja aliyepo sasa Massimiliano Allegri ataondoka kwenye klabu hiyo. (Tuttosport - in Italian)
 
Leicester wanaweza kuiomba Monaco kumfanya Mreno Adrien Silva mwenye umri wa miaka 29 anayeicheziea kwa deni kuhamia huko kabisa ili kupunguza gharama ya pauni milioni arobaini (£40m)- ambayo ndiyo kiwango cha thamani ya mchezaji wa safu ya kati ya Ubelgiji Youri Tielemans, mwenye umri wa miaka 21, ambaye anacheza kwa deni katika Foxes nchini Ufaransa. (Leicester Mercury)
 
Meneja wa kikosi cha vijana cha Borussia Dortmund Lars Ricken anasema klabu hiyo itaendelea kuwalenga vijana wa Kiingereza baada ya kuhfanikiwa kusaini mkataba na winga wa England Jadon Sancho, R Kelly avunja ukimya mwenye umri wa miaka 18, kutoka Manchester City. (Evening Standard)
 
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Mfaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 24, anasema kuwa hana uhakika juu ya hatua atakayoichukua baada ya kumalizika kwa msimu mrefu wa deni katika AC Milan . (France Football - in French)
 
Hull wameazimia kusaini mkataba na mlinda lango wa Reading Luke Southwood, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni mchezaji wa mkopo katika Ligi ya taifa kutoka Eastleigh. (Mail)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…