Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NDOA YAFUNGWA WODINI BAADA YA BWANA HARUSI KUSHAMBULIWA NA KULAZWA: Wanandoa Muneer Hercules na Maryam Kallile wameweka historia kwenye hospitali ya Gatesville Melomed nchini Afrika Kusini kwa kuwa wanandoa wa kwanza kufunga ndoa kwenye wodi za hospitali hiyo kufuatia sherehe iliyofanyika Jumapili Machi 10. Wawili hao walilazimika kufunga ndoa hiyo baada ya Muneer kushambuliwa na majambazi siku ya Jumamosi akiwa nyumbani kwenye jiji la Cape Town na kujeruhiwa hali iliyopelekea kulazwa hospitalini siku moja kabla ya siku ya kufunga ndoa. Iliulazimu uongozi wa hospitali hiyo kuruhusu ndoa hiyo ifungwe kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Muneer na baada ya kukisafisha chumba hicho waliwaruhusu watu wachache wa karibu na familia hiyo kusherehekea kidogo bila kuathiri utaratibu wa hospitali. Hercules ameruhusiwa kutoka hospitalini mapema hii leo baada ya hali yake kuimarika.
 
Zidane, anarejea Madrid, miezi 10 baada ya kuipa ubingwa wa Ulaya mara 3 mfululizo, akiwa na kibarua kigumu cha kurejesha makali ya timu hiyo, iliyoondolewa katika michuano ya klabu bingwa Ulaya na Ajax kwa kipingo cha aibu cha 4-1. Katika ligi kuu ya Hispania "Laliga" Madrid kwa sasa iko katika nafasi ya tatu, iizidiwa pointi 12 na vinara wa ligi hiyo, Barcelona.
 
Zidane alijiuzulu kuifundisha Madrid mwezi May mwaka jana kutwaa ligi ya mabingwa kwa kuifunga Liverpool, Julen Lopetegui alichukua nafasi yake kabla nay eye kutiuliwa muda mfupi kabla ya michuano ya kombe la dunia, kufuatia kukubalia kuifundisha timu ya taifa ya Hispania katika michuano hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…