Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Xherdan Shaqiri

Staa mfupi wa kimataifa wa Uswisi. Huyu ndiye ambaye bado anaendelea kukipiga miongoni mwa mastaa waliopo katika orodha hii. Anaweza kucheza katika pambano la leo katika uwanja wake wa zamani Allianz Arena.
 
Alianza maisha yake ya soka katika klabu ya FC Basel ya kwao Uswisi na alitwaa mataji matatu ya Ligi kabla ya kwenda Bayern Munich. Akiwa na Bayern Munich alitwaa mataji manane ya ndani na mengine ya nje licha ya kucheza kwa dakika chache. Januari 2015 alihamia Inter Milan kwa dau la Euro 15 milioni.
 
Miezi saba baadaye alitua Stoke City ya England kwa dau la pauni 12 milioni ambalo lilikuwa rekodi ya klabu hiyo. Baada ya Stoke City kushuka mwaka 2018 alitua Liverpool kwa dau la pauni 13 milioni.
 
Sababu Zinazopelekea Mashabiki kumkataa Boy Friend Mpya wa Nicki Minaj. - Kenneth Petty yupo kwenye orodha ya watu hatari zaidi waliotenda makosa ya Kingono 'Level two registered sex offender' mjini New York, Polisi wanaimani ni mtu atakaye fanya makosa hayo tena na atakuwa kwenye hio orodha maisha yake yote. - April 1995 Kenneth Petty alihukumiwa kifungo cha miaka 4 na miezi mitano jela kwa kosa la kutaka kufanya ubakaji dhidi ya binti mwenye umri chini ya miaka 16. Muda huo Kenneth alikuwa na miaka 15. - Kenneth alikubali kosa la kuua bila kukusudia baada ya kumpiga risasi Lamont Robinson mwaka 2002, alitumikia miaka saba jela, mitatu chini ya uangalizi wa polisi na alikuwa mtu huru rasmi May 2018. - Nicki Minaj anamjua Kenneth toka utotoni ndio maana anaimani naye na anamfahamu kuliko mashabiki zake, Aliwahi kujibu kuwa >Watu kwenye Internet hawawezi kuendesha maisha yangu, nyie wenyewe hamuwezi kuendesha maisha yenu
 
VIOJA VYA KALE: KODI YA NDEVU : Kule Uingereza miaka ya 1533 alikuwepo mfalme mmoja alijulikana kama King Henry VIII. Mfalme huyu kimtaa mtaa vijana wangemuita bedui. Kwanza alikuwa analala na sururu ndogo. Alikuwa analala na sururu kwa sababu hakuwahi kumwamini sana kila mtu aliyekuwa karibu yake hasa hasa wake zake. : Alifanikiwa kuoa wake 6 kwa nyakati tofauti tofauti. Wawili walionyongwa kutokana na kushukiwa na uzinzi, ambapo mmoja wao kaka yake aliuawa pia kwa kuhisiwa kula njama na mke wa mfalme ili kumuua mfalme. Mmoja alidumu nae miaka 24, wawili walipewa talaka na mmoja alifariki. : Mfalme huyu pia aliidhinisha kodi ya ndevu. Kwa mwanaume yeyote mwenye ndevu lazima ulipe kodi. : Mbali na historia yake ya kibabe, kwenye masuala ya dini hakuachwa mbali. Kumbukumbu zinasema huyu ndiye mfalme wa kwanza kabisa kumjibu Martin Luther Sir aliyeandika majarida na kuanzisha midahalo ya kulipinga kanisa katoliki. : Mfalme Henry ndiye aliyekuwa mtawala wa kwanza wa Kiingereza kukubali biblia ya Great Bible ambayo ndiyo biblia ya kwanza ya kiingereza kusomwa makanisani. : Baadae alitangazwa kuwa mlinzi wa Imani na Papa Leo X. Hata hivyo kanisa lilimfutia uwezo wa kupokea sakramenti kama komunyo na kumtenga kama mkatoliki. : Hii ilitokea mara baada ya kumshurutisha Papa amsaidie kutoa talaka kwa mkewe Catherine. Papa aligoma. : Mgomo huo ndio uliotenganisha kanisa la Anglican (Waanglikana) na ukatoliki na Mfalme huyo akajitangaza kuwa kiongozi wa kanisa la Kiingereza (Anglican)
 
Mwanamuziki Jennifer Lopez amevishwa Pete ya Uchumba kwa mara ya 5 na mchumba wake Alex Rodriguez. Mara ya kwanza Jlo alichumbiwa mwaka 1997 na Ojani Nia penzi halikudumu sana baada ya mwaka wakaachana. Cris Judd aliyekuwa dansa wake kushika hatamu ndani ya mwaka mmoja tu penzi chaliii. Mwingine aliyewahi kulamba asali na pete akamvisha ni Muigizaji Ben Affleck couple iliyopewa jina Bennifer ndoa yao ilidumu kwa miaka miwili tu na kuvunjika. Baadae Jlo alichumbiwa na Muimbaji Marc Anthony na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili mapacha
 
Cristiano Ronaldo alisajiliwa ili kuipatia Juventus ushindi wa ligi ya mabingwa - na huenda akafanikisha ndoto hiyo.
Nyota huyo raia wa Ureno alionesha umahiri wake katika soka ya barani ulaya baada ya kuiwezesha klabu hiyo ya Italia kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuinyuka Atletico Madrid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…