Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MASHABIKI wa Manchester United Jumapili walingoja sana kuona timu yao ikipindua matokeo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kama walivyofanya huko kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki iliyopita.
 
Man United ikasubiri kuona bao likirudi, halikurudi, kufumba na kufumbua, wakapigwa chuma cha pili kwa penalti ya Pierre-Emerick Aubameyang. Hadi hapo, mechi ikawa imekwisha na Man United, ambao ni wababe wa kupindua matokeo kwa msimu huu, jahazi lao lilizama moja kwa moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…