Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Wolves– mechi 17, pointi 11

Wolverhampton Wanderers imekuwa ikipambana kwelikweli na kuzipa shida timu zenye uzito mkubwa kwenye Ligi Kuu England msimu huu, jambo hilo limeiondoa kwenye presha kubwa. Kikosi hicho kinachonolewa na Nuno Espirito Santo kwa msimu huu kimevuna pointi 44 katika mechi 30 ilizocheza, lakini pointi 11 imezipata katika mazingira magumu baada ya kutanguliwa kufunga kwenye mechi.
 
Wolves imetanguliwa kufungwa kwenye mechi 17, lakini imeshinda mara mbili na kutoa sare tano katika mechi hizo jambo linaloifanya ijikusanyie pointi 11.
 
4. West Ham– mechi 19, pointi 12

Kama ilivyo kwa Wolves, West Ham United, nayo imekuwa na mambo matamu kabisa kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Kwenye mechi zake 30 ilizocheza imejikusanyia pointi 39. Katika mechi hizo, West Ham United imetanguliwa kufungwa bao kwenye mechi 19, lakini kati ya hizo iliweza kuokoa pointi 12, ikitoka nyuma na kushinda mara tatu na ilichomoa na kupata sare mara tatu.
 
3. Arsenal– mechi 12, pointi 12

Arsenal ya Unai Emery si kwamba inafurahia sana msimu wake huu kwenye Ligi Kuu England, lakini inapambana kwa nguvu zote na sasa ipo kwenye Top Four ya mikikikimikiki hiyo. Hapo Jumapili, iliichapa Manchester United 2-0 uwanjani Emirates na kufikisha pointi 60 zinazoifanya kujitutumua kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.
 
Lakini pointi zake hizo 60 ilizopata, 12 iliziokoa kutoka kwenye mazingira ya kuanza kufungwa kwenye mechi zake za ligi. Arsenal kwenye ligi ya msimu huu imetanguliwa kufungwa kwenye mechi 12, lakini imeokosa pointi 12, ikishinda tatu na kutoa sare mara tatu.
 
Back
Top Bottom