Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aisee
 
Kocha wa Arsenal, Unai Emery amesema atajisikia fahari kushinda taji lake la kwanza akiwa na klabu hiyo baada ya jana timu yake kupindua matokeo ya kichapo cha 3-1 na kufuzu robo fainali ya Europa League kwa jumla ya mabao 4-3.
 
Arsenal ilifanikiwa kuifunga Rennes ya Ufaransa mabao 3-0 yaliyofungwa na Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga mawili dakika ya 5 na 72 na lingine likifungwa na Ainsley Maitland-Niles dakika ya 13.
 
Kocha huyo anaona hiyo ni nafasi yao ya kupata tiketi ya ziada kutinga Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kama watachukua ubingwa wa Europa League kwani kupata nafasi hiyo kwa kutegemea ubingwa wa Ligi Kuu England ni kazi ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…