Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kupiga Hat trick ya juzi, Ronaldo pia alikuwa amemfikia hasimu wake Lionel Messi katika ufalme wa wachezaji waliofunga hat trick nyingi zaidi katika michuano hiyo. Juzi ilikuwa ni hat trick yake ya nane akiwa amemfikia Messi ambaye mpaka kufikia jana kabla ya pambano dhidi ya Lyon alikuwa na idadi hiyo ya Hat trick.
 
Kwa kupiga Hat trick ya juzi, Ronaldo pia alikuwa amemfikia hasimu wake Lionel Messi katika ufalme wa wachezaji waliofunga hat trick nyingi zaidi katika michuano hiyo. Juzi ilikuwa ni hat trick yake ya nane akiwa amemfikia Messi ambaye mpaka kufikia jana kabla ya pambano dhidi ya Lyon alikuwa na idadi hiyo ya Hat trick.
 
Ronaldo na Messi wamewaacha mbali mastaa wanaofuatia kwa idadi kubwa ya Hat trick ambao ni Filippo Inzaghi, Mario Gomez na Luiz Adriano ambao kila mmoja ana hat trick tatu katika michuano hiyo maarufu barani Ulaya. Na sasa Atletico inakuwa timu ya pili kwa kufungwa mabao mengi na Ronaldo katika historia ya soka. Kwa mabao yake matatu ya juzi, Ronaldo anakuwa ameifunga Atletico mabao 25 huku timu ambayo ameifunga zaidi ikiwa ni Sevilla ambayo ameifunga mabao 27.
 
Ronaldo pia ameifunga Atletico mabao ya ugenini 10 huku akiwa amezifunga Sevilla na Barcelona mabao 12 kila moja ugenini. Ronaldo ameifunga Atletico mabao mengi zaidi ya penalti kuliko timu nyingine yoyote ile huku akiwa ameifunga penalti zote tisa alizopiga katika jezi za Real Madrid na kisha Juventus.
 
Ronaldo aliyenunuliwa kwa dau la Pauni 80 milioni kutoka Real Madrid katika dirisha kubwa lililopita la majira ya joto mara baada ya kumalizika kwa pambano la juzi alitamba mabao anayofunga ndio sababu kubwa iliyopelekea Juventus imnunue.

“Ndio maana Juventus walinileta hapa, kwa ajili ya kuwasaidia vitu ambavyo hawajawahi kufanya awali. Hii ndio akili ambayo inaweza kukusaidia kutwaa ubingwa wa Ulaya. Mimi nafanya kazi yangu na nina furaha sana leo. ulikuwa usiku wa maajabu. Siku zote Atletico ni timu ngumu kupambana nayo lakini mara zote tupo imara na tumethibitisha hilo,” alisema Ronaldo.
 
Tulihitaji usiku maalumu na ndivyo ilivyokuwa, sio tu kwa mabao yangu bali kwa timu nzima. Huu ndio moyo wa kucheza katika Ligi ya mabingwa. Tunajivunia sana hilo,” aliongeza staa huyo wa zamani wa Manchester United. Katika pambano hilo, kamera zilimuonyesha mpenzi wa Ronaldo, Georgina Rodriguez akilia jukwaani akiwa pamoja na mtoto wa kwanza wa Ronaldo Cristiano Junior, ambaye anakipiga katika timu ya watoto ya Juventus.
 
1552654377089.png
 
WANAWAKE mkoani Tabora wamekuwa wakitumia tumbaku na ugoro ambayo huiweka sehemu za siri ili kupunguza hamu ya tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa uchunguzina mahojiano yaliyofanywa na shirika la habari la Uingereza (BBC), tabia hiyo imezoeleka sana miongoni mwa wanawake wasio na wenza wao, wakiwemo wajane. Hata hivyo, kitendo hicho kinasemekana huwa hakina madhara kwa afya zao.

Wanawake, hususan wasio kuwa katika uhusiano na wanaume ama kuolewa, hutumia njia mbalimbali kumaliza hamu zao.
”Mimi ni mjane, natumia tumbaku katika kumaliza hamu zangu kwa sababu sina mwanaume na wala sitaki mwanaume mwingine. Kwa wiki naweka mara mbili,” anasema Zaituni Shaban, mmoja ya wanawake wanaotumia tumbaku kwa kuziweka sehemu za siri.

Mwanawake mwingine, Asha (si jina lake halisi) amesema anatumia tumbaku kwa sababu alikimbiwa na mwanaume wakati ana ujauzito.
”Kwa kweli sitaki kusikia tena wanaume, mi nitabaki na tumbaku, maana nikitumia hamu yote inaisha sina haja tena,” anasema.

Wanawake wote waliozungumza wanakiri kuwa matumizi ya tumbaku sehemu za siri huwasaidia kumaliza hamu ya tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa wanawake hao, huchukua majani makavu ya tumbaku kisha kuyatangwa na baada ya hapo huchanganya na mafuta kidogo pamoja na magadi, na mara nyingine hutumia ugoro kufanya mchangayiko huo. Baada ya hapo huweka sehemu za siri na kisha hupata mwasho ambao humaliza haja ya tendo la ndoa.

”Mi huwa napaka mara mbili kwa wiki na huwa naweka kwa muda kidogo kabla ya kuondoa na kisha napata mwasho, na wala sipati maumivu yoyote nikimaliza matamanio yangu ya kufanya tendo la ndoa mambo yanakuwa yameisha,” anasema Zaituni.
Kwa kawaida wanawake hawa baada ya kupaka tumbaku ama ugoro sehemu za siri husikia kama wamekutana kimwili na wanaume.

Katika kijiji cha Ugala, suala hili ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake lakini kwa upande wa wanaume si wengi wanalijua na wanaojua wanasema kuwa imekuwa siri baina ya wanawake tu.
“Mimi nimekuwa nikisia lakini mara nyingi kwa bahati mbaya wakiongea na nikuwauliza, wanasema ni siri yao baina ya wanawake na si wanaume,”anasema anasema mzee Usantu mmoja wa wakazi wa kijiji hicho cha Ugala.

Kwa mujibu wa baadhi ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu zao za siri, wanasema hawajawahi kupata tatizo lolote kiafya.
Lakini mtaalamu wa magonjwa ya kinamama anasema kuwa baadhi ya wanawake wanaokutwa na viashiria vya saratani hasa ya kizazi wamekuwa na historia ya kutumia tumbaku sehemu za siri.

“Hatuna utafiti wa moja kwa moja lakini data za kwetu hapa wakati tunawahoji tabia za mazoea walizonazo, baadhi wamekiri kutumia tumbaku, hivyo hiyo inaweza kuwa miongoni mwa sababu, ” anasema daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Matumizi haya ya tumbaku kwa asilimia kubwa yamechangiwa na uelewa mdogo wa wanawake wa kijiji hicho juu ya madhara ya kiafya wanayoweza kupata.
CHANZO: BBC SWAHILI.
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]zamani wa mjini walikuwa wanatumia "kologeti" dawa ya meno
 
Back
Top Bottom