Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchezaji wa Hull City Jarrod Bowen amekataa ofa ya euro milioni 12 kuhamia Cardiff City baada ya klabu hiyo kujaribu kumsaini wakati Emiliano Sala alipopotea katika mkasa wa ndege, lakini hajathibitishwa kuwa amefariki.
 
Meneja wa Leeds United Marcelo Bielsa huenda akaondoka uwanja wa Elland Road ikiwa klabu hiyo haitafuzu kujiunga na ligi ya Primia, kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa klabu hiyo Danny Mills. (Talksport)
 
Nia ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May kuona nchi yake inajiondoa katika Umoja wa Ulaya (EU) imegonga mwamba na kesho Wabunge wa Uingereza watapiga kura ambazo dalili za awali zinaonyesha kuwa zitakuwa za kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo.
 
Sababu hasa za kisiasa na kiuchumi ndizo zinaonekana zimechochea kiu ya kundi kubwa la raia wa Uingereza kutaka kuona wanajiondoa katika Umoja wa Nchi za Ulaya kwa kile wanachoamini kwamba hawanufaiki na uwepo wao kwenye Jumuiya hiyo tofauti na mawazo ya May.
 
Hata hivyo uamuzi kama huo unavyochukuliwa ni lazima uwe na faida na hasara, matokeo ambayo huenda sambamba ingawa yale yenye manufaa zaidi kwa mtazamo na hisia za wahusika ndio huchukuliwa.
 
Ikiwa Uingereza itajiondoa rasmi kwenye Jumuiya ya Ulaya, mchezo wa mpira wa miguu (soka) ambao ni moja ya utambulisho mkubwa wa visiwa vinavyounda nchi hiyo hasa England, ni miongoni mwa sekta zitakazopata athari hasi na uamuzi huo.
 
Inawezekana upande wa kisiasa na kiuchumi nchi hiyo ikanufaika lakini Ligi Kuu ya England (EPL) ambayo inatajwa kama Ligi Bora na maarufu zaidi ya soka duniani ukakumbana na anguko litakaloishusha hadhi na kutoa nafasi kwa ligi nyingine kama ile ya Hispania (La Liga), Ujerumani (Bundesliga), Italia (Serie A) na Ufaransa (Ligue One) kushika hatamu.
 
Kupungua kwa nyota wa kigeni

Kwa sasa kuna urahisi kwa nyota wengi wa soka kutoka mataifa mbalimbali barani Ulaya kucheza Ligi Kuu ya England wakitumia mwavuli wa hati ya kusafiria ya Jumuiya ya Ulaya lakini pia kulegezewa masharti ya kupata vibali vya kazi nchini humo.
 
Nyota wengi wamekuwa wakipata urahisi wa kucheza kwa kutumia kanuni ya kuhesabika kama wachezaji wa nyumbani kutokana na kupitia kwenye vikosi vya vijana vya klabu zinazoshiriki ligi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…