Mamlaka husika ni lazima zichukue hatua kukabiliana na suala hilo kwani hata kama biashara hiyo ikiwa ni sehemu ya watu kujikwamua kiuchumi, lakini wanaoihitaji ni lazima washauriwe, kuelekezwa na wao kufuata hatua kwa hatua yale wanayopaswa kuyafanya ili kuepuka madhara.
Biashara ya petroli na gesi ina miongozo yake iliyowekwa mahsusi ili kukabiliana na hatari zake, na mara nyingi ni matukio ya moto, hivyo zifuatwe kikamilifu.
Viongozi wa vijiji au mitaa wawe jicho la kwanza katika kusimamia na kutazama usalama wa wale wanaofanya biashara hiyo ambao ni sehemu ya wale wanaowaongoza kwani endapo hatari yoyote itajitokeza athari zake huanzia katika kijiji au mtaa husika.
Mamlaka husika ni lazima zichukue hatua kukabiliana na suala hilo kwani hata kama biashara hiyo ikiwa ni sehemu ya watu kujikwamua kiuchumi, lakini wanaoihitaji ni lazima washauriwe, kuelekezwa na wao kufuata hatua kwa hatua yale wanayopaswa kuyafanya ili kuepuka madhara.
Mbali na hilo, kwa wananchi wenyewe nao wanapaswa kuchukua tahadhari wanapohifadhi mafuta ya petroli na mengine yaliyo hatari kwa usalama wa watu na mali.
Itashangaza kuona mtoto mchanga au hata wale waliofikisha miaka zaidi mitano walazwa katika chumba chenye petroli ambao kujinusuru endapo moto utalipuka katika tukio kama la Same itawawia vigumu kujiokoa.
Ulinzi wa usalama wako na mali unapaswa kuanza na wewe mwenyewe kabla ya kushikiwa kitabu chenye orodha ya sheria, taratibu na miongozo ya kukuweka salama dhidi ya jambo lolote.
Tunawapa pole walioondokewa na wapendwa wao katika tukio la Same, lakini hilo linapaswa kuwa somo kwa wengine wanaendelea na biashara ya mafuta ya kidebe. Tunawasihi kuchukua tahadhari kwani inaweza kumtokea yeyote wakati wowote.
Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann anajuta kutojiunga na Barcelona msimu uliopita na sasa anatamani kujiunga na klabu hiyo ya Nou Camp. (L'Equipe - in French)
Lakini licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema yuko tayari kujiunga na klabu nyengine za Ulaya ikiwemo Barcelona, klabu hiyo ya Catalan haina haja naye.. (ESPN)
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich huenda akatumia likizo ya kimataifa kumfuta kazi kocha Maurizio Sarri baada ya kulazwa na Everton siku ya Jumapili. (Express)
Kiungo wa kati wa Bayern na Colombia James Rodriguez, 27, hataki kusalia mjini Munich zaidi ya kipindi chake cha mkopo kutoka Real Madrid, kinachoisha mwisho wa msimu huu. (Marca)
AC Milan huenda ikazuiwa na thamani ya Everton ya Yuro milioni 70 za mchezaji wa klabu hiyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Brazil Richarlison. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa klabu ya Benfica Joao Felix anasema kuwa anafurahia kuwa katika klabu hiyo , licha ya hamu kutoka kwa klabu za Manchester United na Chelsea.
Liverpool wamewasiliana na Benfica kuhusu uwezekano wa kuvunja rekodi ya dunia katika usajili wa beki wa kati wa Ureno Francisco Reis Ferreira, 21. (Record, via Metro)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ataendelea kuifunza timu hiyo kwa muda mrefu baada ya nahodha wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer kusema kuwa huenda akaifunza Bayern Munich. (Liverpool Echo)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ataendelea kuifunza timu hiyo kwa muda mrefu baada ya nahodha wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer kusema kuwa huenda akaifunza Bayern Munich. (Liverpool Echo)