Tanzania yetu
Duh!!Moja ya matukio ya huzuni na kusikitisha yaliyotokea wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro, wiki iliyopita, ni lile la moto lililosababisha vifo vya watu saba. Moto huo uliotokea katika Kijiji cha Marwa, Kata ya Ruvu, Jumatano iliyopita ulitokana na biashara ya petroli iliyokuwa ikifanyika nyumbani, na kwa kuwa haikuwa ikizingatia taratibu za usalama wakati muuzaji akimpimia bidhaa hiyo mteja wake karibu na jiko la mkaa, moto uliripuka na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo.
SawasawaTunawapa pole walioondokewa na wapendwa wao katika tukio la Same, lakini hilo linapaswa kuwa somo kwa wengine wanaendelea na biashara ya mafuta ya kidebe. Tunawasihi kuchukua tahadhari kwani inaweza kumtokea yeyote wakati wowote.