Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa upande wa Solskjaer kwenye mechi hizo 19, ameshinda 14, sare mbili na amepoteza mechi tatu. Kikosi hicho cha Man United chini yake kimefunga mabao 40 na kufungwa 17. Kwa maana hiyo, kikosi hicho cha Solskjaer kimevuna pointi 44, moja zaidi ya alizovuna Emery huko kwenye kikosi cha Arsenal katika mechi zake 19 za mwanzo.
 
Kwenye kipengele cha tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, Emery kikosi chake kina chanya ya 21, wakati Ole kikosi chake kina chanya ya 23. Kama ingekuwa kushinda mechi zote, basi Ole angepaswa kuvuna pointi 57, lakini kwa 44 alizopata hiyo ina maana chama lake la Old Trafford limepoteza pointi 13.
 
Vichapo vitatu vya Ole Gunnar alikumbana navyo, dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kisha dhidi ya Arsenal Ligi Kuu England na Wolves kwenye robo fainali ya Kombe la FA.
 
Lakini, shabiki mwingine alisema: “Huo ni mzaha. Hebu cheki kwa sasa tumekuwa hata na uhakika tunakwenda kukabiliana na timu za Top Six tukiwa na imani tutashinda ikiwa ni tofauti na miaka mingi iliyopita.”
 
Huo ndio mjadala uliopo huko na mwingine alikuja kuhitimisha kwa kusema Solskjaer hana uzoefu kwenye ukocha kama aliokuwa nao Emery, hivyo anachokifanya huko Man United akiwa kocha wa muda hakina ubishi, kinahitaji kupewa pongezi.
 
Winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi - ambaye hajaanzishwa mechi yoyote ya ligi ya Premia anasema kuwa ameshangazwa baada ya kupata wito katika timu ya Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alishirikishwa katika kikosi cha timu ya Uingereza siku ya Jumatatu kwa maandalizi ya mechi za kufuzu kwa michuano ya Yuro 2020 dhidi ya Jamhuri za Czech na Montenegro.
 
Alikuwa na timu ya Uingereza iliopo na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21, baada ya kupata mwaliko wake wa kwanza wiki iliopita, ambapo aliambiwa kwamba ataichezea timu kubwa na mkufunzi wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Aidy Boothroyd.
 
''Nilishangaa sana na nilipoambiwa kwamba nimepandishwa hadi timu kuu sikuamini'', Hudson Odoi aliongezea.
Hudson Odoi alishirikishwa katika kikosi hicho baada ya Luke Shaw, John Stones , Fabian Delph na Ruben Loftus Cheek kujiondoa.
Uingereza itacheza dhidi ya Czech katika uwanja wa Wembley siku ya Ijumaa, 22 Machi na wataelekea Montenegro siku ya Jumatatu , 25 Machi.
 
Mizizi ya Callum James Hudson Odoi
Alizaliwa tarehe 7 mwezi Novemba 2000 kutoka kwa wazazi wake Bwana na bi Bismark Odoi katika eneo la Uingereza la Wandsworth .
Ni mtoto wa pili katika wavulana watatu.
Familia ya Callum Hudson ina mizizi ya taifa la Ghana. Babaake Bismark Odoi ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Ghana Hearts of Oak .
 
Alikuwa na umri wa miaka 17 na siku 75 wakati alipoichezea timu hiyo dhidi ya Hungary kwa mara ya kwanza 2006 baada ya kukosa kucheza katika ligi kuu.
Mechi 11 kati ya 19 alizoshiriki Hudson Odoi akiichezea Chelsea msimu huu alicheza kama mchezaji wa ziada huku akianzishwa katika mechi za mashindano ya makombe.
Katika mechi nane alizoanza, hatahivyo amefunga magoli manne na kutoa pasi nne zilizosaidia kufungwa kwa magoli.
 
Chelsea yakataa kumuuza
Akikasirishwa na muda aliopewa kucheza mechi katika klabu ya Chelsea.
Hudson Odoi aliomba uhamisho mwezi Januari kufuatia hamu ya dau la £35m kutoka kwa Bayern lakini Chelsea ilikataa kumuuza.
Mapema mwezi huu , mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri alisema kuwa ni hatari kumweka katika shinikizo kinda huyo akisema kuwa atakuwa mchezaji mzuri atakapofikisha umri wa miaka 22 au 23.
 
Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo amechukuliwa hatua za kinidhamu na Uefa baada ya kushangilia 'visivyo' ushindi wa klabu yake dhidi ya Atletico Madrid katika mchuano wa ligi ya mabingwa wa kufuzu kwa awamu ya robo fainali juma lililopita.
Nyota huyo wa 34 alionekana kumkejeli meneja wa Atletico, Diego Simeone, huku akiwageukia mashabiki wa klabu hiyo na kujishika sehemu zake za siri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…