Bale alisema kwenye kipindi chake cha utoto amekua kwa kuwatazama mastaa Thierry Henry na Dennis Bergkamp walipokuwa pamoja huko kwenye kikosi cha Arsenal na alitumia wachezaji hao kama dira katika kuendeleza soka lake.

Nilikuwa nikimtazama pia Dennis Bergkamp. Walikuwa na timu nzuri. Nafahamu mashabiki wa Tottenham hawawezi kulifurahia hili nimekuwa nikiishabikia Arsenal!.”
Staa huyo kwa sasa anatajwa huenda akarudi kwenye Ligi Kuu England akiwindwa na Manchester United na hata timu yake ya zamani ya Spurs na haifahamiki mashabiki wa timu hiyo watampokeaje baada ya kukiri huku yeye tangu utoto wake alikuwa akiishabikia Arsenal.