WAKALA Mino Raiola wa mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba halali. Anahangaika usiku na mchana kuhakikisha mteja wake anapata timu mara dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa.
Mshambuliaji huyo amekuwa mguu nje ndani tangu enzi ya Kocha Jose Mourinho, lakini sasa anasema anataka kuondoka klabuni hapo na hesabu zake ni kwenda ama Hipania au Italia.
Baada ya kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane kurejea kikosini, alisema anataka kufumua kikosi chake na alitaja listi ya nyota anaowataka akimtaja na Pogba, ndipo alipomchanganya akili na sasa anamsumbua wakala wake amfanyie mipango.