Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ole amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kufanya kazi Old Trafford asubuhi ya Alhamisi na hilo limekuja baada ya kuingoza timu hiyo ikipoteza mara moja tu katika mechi 13 ilizocheza kwenye Ligi Kuu England.
 
Mwingereza huyo alitumia ukurasa wake wa Twitter kuandika: "Nimefurahishwa na Ole. Sidhani kama hili lingetokea kama asingechaguliwa. Matokeo na kile alichokifanya kwenye timu ni kubwa sana tangu alipowasili, hivyo amestaahili. Anahitaji tu kusaidiwa kwenye kusajili kwa maana ya kupewa pesa na mambo mengine muhimu.”
 
Mapema tu Ole aliripotiwa kutaka kunasa makinda wa Kingereza, Callum Hudson-Odoi, Jadon Sancho na Declan Rice huku kwenye orodha hiyo kukiwamo wakati wengine Aaron Wan-Bissaka na Harry Maguire, lakini Man United itabidi iuze kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…