Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye taarifa yake, Solskjaer alisema: “Tangu siku ya kwanza niliyowasili hapa, nilijiona nipo nyumbani katika klabu hii spesho. Niliheshimika sana kuwa mchezaji wa Manchester United na kisha nilianza kazi yake ya ukocha mahali hapa.
 
Hii ni kazi ambayo siku zote nilikuwa na ndoto nayo na hakika nimefurahi sana kwa kupata nafasi hii ya kuingoza klabu hiyo kwa muda mrefu na natumaini tutaendelea kupata mafanikio kwa ajili ya mashabiki wetu matata kabisa.”
 
Zaidi ya kiwango na matokeo, Ole ameleta pia uzoefu wenye afya kama mchezaji na kocha na kuwapa wachezaji makinda nafasi ile wanayostahili ikiwa ni utamaduni wa klabu. Hii ina maana kwmaba ni mtu sahihi wa kuipeleka mbele Manchester United.
 
Nataka kumshukuru Ole na benchi lake la ufundi kwa kila kitu walichokifanya hasi kufika sasa na hakika amestaahili kuchaguliwa. Mashabiki na kila mtu klabuni wanampa sapoti na inavyoonekana atatufikisha kuna tunakohitaji kwenda kwa ajili ya kutengeneza historia mpya katika klabu yetu.”
 
Wakati Solskjaer anachukua timu, Man United ilikuwa nafasi ya sita kwenye msimamo, pointi 11 nyuma kuifikia Top Four, lakini tangu wakati huo amepoteza mechi moja tu kati ya 13 kwenye ligi alipocheza na Arsenal na timu ipo nyuma kwa pointi mbili kuingia nne bora inayotoa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Rekodi yake ya mechi zote, Solskjaer ameshinda 14, sare mbili na kupoteza mara tatu, huku timu yake ikifunga mabao 40 na kufungwa 17
 
455218691_248797.jpeg
 
Back
Top Bottom