Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*Wanaume mpunguze ukali kwa wake zenu ipo siku mtalia kama rafiki yangu huyu, yaliyomkuta ni kibokooo,*[emoji15][emoji116]

jamaaa alikuwa mkali sana kwa mkewe kiasi kwamba kosa dogo anafoka .Nakutoa maneno hata some time kumpiga. Jamaa juzi kaumwa sana kupelekwa hospital akaambiwa akalete mkojo ili wajue anaumwa nanini.
jamaa asubuhi na mapema kachukua mkojo wake vizuri kauweka kwenye kichupa cha hospitali alichopewa. Akauacha juu ya kabati, ili ajiandae kuvaa na kwenda hospitali. Bahati mbaya mkewe kupanga panga vitu kichupa kikadondoka mkojo ukamwagika wote. Kwa kuogopa kipigo faster mkewe kachukua kile kichupa akatia mkojo wake akakirudishia pale, then Akauchuna kimya. Jamaa kupeleka hospitali majibu yakatoka kuwa ana UTI na mimba ya miezi mitatu. sasa jamaa anahisi karogwa kumbe kajiroga mwenyewe. Hivi yuko njiani kuelekea sumbawanga[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]na mimi nmemwambia ukizubaa utajifungulia njiani mtoto njiti[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji2816][emoji2816][emoji2816]
 
Dear short people, please don't be short for nothing, Help us check the root of our problem in this country[emoji30][emoji30][emoji30][emoji30][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Babu alisema Ukiona mapenzi hayakuumizi, ushakuwa malaya! [emoji573][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
anonymous poll

True [emoji23] – 110
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106] 92%

False – 5
[emoji3503] 4%

[emoji22] – 5
[emoji3503] 4%

[emoji186] 120 people voted so far.
 
Vituko ! Mapacha wawili wa kiume wanaofanana(identical twins) wamewatoa jasho madaktari na mahakama nchini Brazil baada ya wote kuuchuna kutajana ni yupi kati yao ni baba halisi wa mtoto aliyezaliwa baada ya mmoja wao kumpa mimba msichana ambaye amejifungua. Msichana husika amekimbilia mahakamani kudai pesa za matunzo ya mtoto baada ya kushindwa kumjua baba halisi wa mtoto wake kufuatia mapacha hao kufanana sana hadi tabia zao hivyo yeye kubaki njia panda . . Baada ya kukimbilia mahakamani, mapacha hao walichukuliwa vipimo ambapo majibu ya madaktari nayo yameshindwa kubaini ni yupi baba halisi wa mtoto kwasababu DNA zao nazo zimeonesha kufanana Kwa asilimia 100% . . Licha ya Mahakama kuomba aliyelala na msichana huyo ajitaje au ambaye hahusiki ajitaje hakuna aliyekuwa tayari kutoa jibu hivyo Mahakama kutoa hukumu jamaa hao wote majina yao yaandikwe kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo wa kike pia Mahakama ikatoa hukumu Kwa mwezi wote kila mmoja atoe pesa dola $60 jumla U$120 zaidi ya laki 270,000 za Kibongo kwa ajili ya matunzo ya mtoto huyo .
 
SIO kazi rahisi sana kuwafurahisha Wazungu katika Ligi Kuu ya England. Kuna mastaa wengi ambao wametamba katika Ligi Kuu England lakini hawakuweza kufikisha mabao 50 katika Ligi Kuu ya England. Wafuatao ni mastaa ambao wameweza kufikisha mabao 50 Ligi Kuu England. Wengine kina Demba Ba na wengineo walichemsha licha ya kuonekana wametamba England.
 
Sadio Mane (Mabao 50+)

Katika pambano la Ligi kuu kati ya Liverpool dhidi ya Cardiff City Oktoba mwaka huu, Mane alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1. Kwa kufanya hivyo, Mane alikuwa mchezaji wa saba kutoka Afrika kufikisha mabao 50. Mabao mengine alifunga na klabu ya Southampton. Katika pambano dhidi ya Fulham Machi mwaka huu Mane alifunga bao moja na kwa kufanya hivyo aliweka pia rekodi ya kuwa mchezaji wa Senegal aliyefunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja.
 
Awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Demba Ba ambaye msimu wa 2011-12 alifunga mabao 16 lakini bao dhidi ya Fulham lilisababisha Mane awe amefunga mabao 17 ndani ya msimu mmoja. Katika orodha hii yeye na swahiba wake wa Liverpool, Mohamed Salah ndio wachezaji ambao bado wanaendelea kucheza pale England.
 
Mohamed Salah (Mabao 50+)

Katika orodha hii huyu ndiye mchezaji aliyefikisha mabao 50 kwa haraka zaidi. Ilikuwa ni katika pambano dhidi ya Crystal Palace Januari mwaka huu. Salah alifikisha mabao hayo baada ya mechi 72. Lakini kwa orodha ya jumla anasimama nyuma ya wakongwe Andy Cole, Van Nisterlooy na Alan Shearer kwa kufikisha idadi hiyo kwa mechi chache.

Anabakia kuwa mwanasoka pekee kutoka Afrika Kaskazini kuingia katika orodha hii.
 
Efan Ekoku (Mabao 52)

Staa wa zamani wa kimataifa wa Nigeria ambaye ni mzaliwa wa Manchester. Aliamua kuitosa England na kukipiga katika Timu ya Taifa ya Nigeria na ndio maana anaingia katika orodha hii. Ekoku ambaye enzi zake alitamba na klabu ya ‘kihuni’ Wimbledon iliyokuwa ikijulikana kama Crazy Gang alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kufikisha mabao 50.
 
Nwankwo Kanu (Mabao 54)

Mmoja kati ya washambuliaji bora kutoka Bara la Afrika ambao waliheshimika Ulaya. Alicheza klabu tatu tofauti Ligi Kuu England zikiwa ni Arsenal iliyomleta kutoka Inter Milan, West Bromwich na Portsmouth alitwaa nayo taji la FA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…