Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UKISHANGAA ya Mussa utayaona ya Philippe Coutinho. Kumbe hata wazungu wanaamini mambo ya Kiswahili. Ndicho kinachoonekana baada ya kisingizio cha nyumba anayoishi staa wa Barcelona, Philippe Coutinho kuonekana kama sababu ya kushuka kwa kiwango chake.
 
Staa huyo wa kimataifa wa Brazil ameshindwa kung’ara tangu alipotua klabuni hapo Januari mwaka jana kwa uhamisho wa Pauni 142 milioni akitokea Liverpool lakini sasa imeelezwa kwamba nyumba ambayo anaishi nchini Hispania ina ‘laana’.
 
Coutinho alitazamiwa kufanya mambo makubwa katika msimu wake huu kamili wa kwanza Nou Camp lakini mambo yamekuwa magumu na sasa anahusishwa kurudi katika Ligi Kuu ya England ambako inasemekana anatakiwa na klabu za Chelsea na Manchester United.
 
Na sasa imebainika kwamba nyumba anayoishi imekuwa na laana kwa wachezaji wengi wa zamani wa Barcelona ambao wamewahi kuishi katika nyumba hiyo na kushindwa kuonyesha makali yao licha ya kutamba katika klabu walizotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…