Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Taarifa kutoka Italia zinafichua Kocha Max Allegri amejipanga kutoa mkono wa kwa heri kwa mastaa kibao wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali ili tu kukifanya kikosi kipumuke na kuweza kufanya usajili mwingine mpya.
 
Kinachoelezwa ni kwamba mpango wa kwanza wa Juventus ni kumsajili staa mwingine wa kiwango cha dunia baada ya kufanya hivyo kwa Cristiano Ronaldo, 34, ilipomnasa kutoka Real Madrid kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana.
 
Kuna orodha ndefu sana ya wachezaji wa kikosi hicho kwa sasa hawachezi mpira katika kiwango cha juu tena hivyo wanataka kuwaondoka. Wachezaji wengine umri umekwenda na wengine dili zao za mikataba zinakwenda ukingoni na hawana mpango wa kuwapa dili mpya.
 
Wachezaji hao 11 ambao wanaweza kuunda kikosi matata wanaotajwa kwamba huenda vichwa vyao vikapitiwa na panga hilo mwishoni mwa msimu huu ni kipa Mattia Perin, mabeki Martin Caceres, Daniele Rugani, Andrea Barzagli, Alex Sandro na viungo Leonardo Spinazzola, Sami Khedira, Miralem Pjanic, Douglas Costa na washambuliaji Paulo Dybala na Moise Kean.
 
Staa wa Kibrazili, Douglas Costa, ameripotiwa kuwindwa na Manchester United na huenda akahusishwa pia kwenye dili hilo Paulo Dybala. Chelsea wao wanamtaka Daniele Rugani, wakati Arsenal macho yao yapo kwa Sami Khedira, wanayedhani anaweza kuwa mbadala mzuri wa Aaron Ramsey.
 
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] aisee kumbe ulikuwa hujui [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…