Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati polisi hawakutaja jina la mwanamke huyo, kampuni yenye makao yake makuu jijini London inayojulikana kwa jina la Detained in Dubai, ilimtaja kuwa ni Laleh Sharavesh, ikisema alimuelezea mke huyo wa mumewe wa zamani kuwa ni “punda”.
 
"Baada ya kurejea nchini (UAE) Machi 10, 2019, hati hiyo iliifanya Idara ya Uhamiaji uwanja wa ndege kumueleza mwanamke huyo suala linalomkabili," polisi ilisema katika taarifa yake.
"Alitakiwa aende kituo cha polisi cha karibu."
 
Uingereza imesema ina mawasiliano na UAE kuhusu kesi hiyo ia inatoa msaada kwa Sharavesh.
"Tunatoa msaada wa kibalozi kwa Sharavesh. Tunafuatilia suala hilo," Waziri wa Mambo ya Nje, Jeremy Hunt aliwaambia waandishi nchini Luxembourg.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…