Bila shaka kwa sasa Barcelona ni klabu yenye maisha ya furaha tele.
Wanaongoza ligi ya Uhispania, maarufu kama La Liga, kwa wigo wa alama 11. Pia wameshatinga fainali ya Kombe la Uhispania.
Kwa vyovyote vile, miamba hiyo ya Uhispania chin ya kocha Ernesto Valverde watakuwa na kila sababu ya kujiamini pale watakapominyana na Manchester United kesho Jumatano katika mchezo wa raundi ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya katika uga wa Old Trafford.