Ushuhuda wa
As Salafiyyu91
Nitaendelea kuwa raia mwema lakini nakumbuka nilishawahi kuzungukwa siku moja na mashine guns za polisi sio chini ya Saba miguu ikitetemeka mwili ulipararaiz kwa mda kamasi nyembamba ziliniteremka ikabidi nipigwe pingu hadi Central
Aisee nikapelekwa Central kwa mahojiano niliojiwa niliulizwa maswali mengi niliojiwa na wapelelezi tofauti tofauti mara naingizwa chumba hiki mara toka ingia pale mpaka nimajihisi nko nchi ya ugenini sipo Tz
Nikasafirishwa kutoka mkoa mpaka Dar nikiwa nimefungwa pingu na mwenzangu mmoja tupo ndani Land Cruiser Mkonga full ving'ora kana kwamba ni msafala wa Rais au viungozi wakubwa wa nchi hali ya kuwa mashine sio chini ya 5 ziko stand by in case kama nitaleta usumbufu wowote tukaletwa mpaka maeneo mikocheni nipapigwa kitambaa cheusi usoni nikawa natubia zambi zangu nikijua siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho kuishi duniani
Nilitukanwa nilisikia kila aina ya tusi nikiitwa mwisho tukapelekwa Tazara kwenye kitengo maalum cha kesi za hatari za ugaidi
Ilichukuliwa Laptop yangu ikasachiwa kilakitu na ICT officers wa upelelezi walikagua mpaka wakachoka sikuwa na hatia yeyote wala hawakukuta kitu chochote zaidi ya notes zangu nilizokuwa nazitumia chuo na assignment na Personal Info zangu
Nilichezea kichapo cha marungu na bonge la njemba miraba minne alikuwa anasema mmeletwa mda huu mmetuzuia kwenda ghetto kuwa DO mademu zetu sasa mtaona cha mtema kuni
Sijawahi kuona mtu akiteswa kama siku hiyo mtu anachapwa Miguuni kwenye nyayo na mafimbo mijeledi wengine wapo uchi kichwa chini miguu juu wanamakovu ya mijeledi sijawahi sikia sauti ya mtu mzima akilia kwa uchungu wa kupingwa fimbo marungu nk kama siku ile aisee
Tukaambiwa sisi hapa tukipata ruhusa tu kutoka kwa mkubwa wetu tunawa shoot sasa hivi mfilie mbali
Mmoja wa akasri akawaanasema hawa jamaa wamekuja kufanya pick Nick wanabahati sana msingerudi uraiani kamwe lakini mungu ni Mwema siku hiyo jamaa walikosa ushahidi kabisa hata ushaidi wa mbali ikapidi tuachiwe na turudishwe mkoani tena kwa usafiri uleule wa land Cruiser tukiwa hatuja fungwa pingu wala kuwekewa Silaha usoni huwezi amini jamaa wakaanza kuongea na sisi stori za kawaida lakini mara ya kwanza wakati wanatuleta ilikuwa ni matusi tu na kukalipiwa huku jamaa wakiwa wako uzo wa mbuzi hawacheki na mtu kama malaika wanaoshika funguo za milango ya moto
Nilikuwa najiuliza lau tungefunguliwa mashtaka na Serikali nani angetutetea mahakamani bila Shaka kifungo cha MAISHA jela ndio ilikuwa stahiki yetu in case tungekutwa na tuhuma
Aisee nakumbuka tulipo ambiwa hamna hatia yeyote Nililia kama mtoto mdogo kwenye gari nikakumbuka kweli wanaokwenda JERA sio wote wenye hatia
Mkuu nilisalimika kwenda jela na kupigwa risasi ya kichwa kamwe kamwe na milele sitokuja kusahau tukio hili.