Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya kutolewa jasho na Brighton kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA, vijana wa Pep Guardiola wameingia fainali, wakipata ushindi mwembamba wa 1-0 katika Uwanja wa Taifa – Wembley, mbele ya washabiki zaidi ya 71,000 kutoka pande zote mbili.
 
Pamoja na kufunga bao mapema kabisa katika dakika ya nne, Man City hawakuwa wale tunaowajua; hawakucheza kwa kasi wala kufanikiwa sana kwenye ushambuliaji wa staili ile yao ya kawaida, na kuna nyakati walitishiwa kufungwa.
 
Lakini pia wamekivuka kihunzi hiki, kikibaki kimoja tu kwa ajili ya kuhifadhi kombe hilo, kwenye mechi ambayo walibahatika kumaliza wakiwa wachezaji 11 uwanjani, baada ya Kyle Walker kumpiga kichwa mchezaji wa timu pinzani, Alireza Jahanbakhsh.
 
Vijana wa Chris Hughton – kocha pekee mweusi katika Ligi Kuu ya England (EPL) waliwabana na kuwatia shinikizo kubwa Man City ‘The Citizens’, lakini walishindwa kabisa kurudisha bao, hivyo kutoa faida kwa City kuitafuta rekodi kwani katika fainali watacheza na ama Watford au Wolves wanaoonekana ‘walaini’
 
Ikiwa Man City wataweka historia hiyo mpya msimu huu, basi mechi hii itawaacha wakiwa kidogo bila raha kwa jinsi walivyocheza hovyo. Hatukuona aina zile za pasi nyingi au mikimbio ya aina yake na vipaji murua vya akina Raheem Sterling na Bernardo Silva ambao wamekuwa wakionekana kwamba hawazuiliki.
 
Ilikuwa moja ya siku zile chache kabisa ambazo City walionekana kutojiamini katika ukuu wao, wakitibuliwa muvu zao mara kwa mara na Brighton. Ikawa ilivyokuwa, City wameshinda na sasa wanasubiri fainali, wakijielekeza kwenye kulibeba kombe hilo.
 
Hata hivyo, hawatajali sana lwa sababu ndoto yao inaendelea na itajulikana mwezi ujao. Tayari kibindoni wanalo kombe moja – Kombe la Ligi, maarufu siku hizi kama ‘Carabao Cup’ walillotwaa Februari pale walipowafunga Chelsea kwa penati 4-3 baada ya kwenda suluhu katika muda wa kawaida.
 
Nayo ilikuwa mechi iliyokuwa na vioja vyake, ambapo golikipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga, katika Uwanja wa Wembley, dakika za mwisho, alikataa uamuzi wa kocha Maurizio Sarri wa kutaka kumtoa, ili aingie kipa Willy Caballero kwa ajili ya kudaka penati.
 
Mwamuzi akiwa amesharuhusu mabadiliko ya kipa, Arrizabalaga alikataa na matokeo yake akaruhusu penati nyingi zaidi kuzama kwenye nyavu za goli lake. Ni kipa ghali kabisa, alinunuliwa kwa pauni milioni 71. Caballero alizuia penati tatu kwenye michuano ya Kombe la Ligi 2016 dhidi ya Liverpool na kuwapa Man City kombe hilo. Safari hii alikuwa kwa wapinzani.
 
Ama tukitazama uwezekano wa kombe la tatu ni la ubingwa wa England kupitia EPL, ambapo wakiwa bado wana mechi nane hivi, wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa kimahesabu, kwani Liverpool wanaoongoza kwa alama 82 wamecheza mechi 33 wakati Man City wana alama 80 kutokana na mechi 32. Ni kitu kilicho ndani ya mikono yao kutetea ubingwa wao huo, na wakifanya yaweza kuwa kombe la tatu.
 
1. CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.

2. CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya wanachama wake

3. CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.

4. Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo hayakufanyika

5. Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni ya shilingi

6. Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.

7. CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

8. Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo yametekelezwa kikamilifu.

9. Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350 lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa kikamilifu.

10. CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.

11. Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.

12. Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa
 
Nne ni pasua kichwa; ubingwa wa Ulaya. Wana kibarua Jumanne ugenini dhidi ya Spurs kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali, ikiwa zote ni timu za England kukutana, tena zikifuatana kwenye EPL pia.
 
Inasikitisha sana. Pole yake nyingi
 
zote tuhuma hizo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…