Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

RAIS MAGUFULI: NILIMUONDOA RPC WA NJOMBE KWASABABU YA MAUAJI YA WATOTO, MSITAFUTE SABABU
-
Rais ahoji, “Inakuwaje anapotea mtoto wa kwanza hadi wa 7, RPC bado upo? Mbona watoto wako hawapotei?”
-
Vilevile Rais Magufuli alisema OCD pia aondoke lakini alitengua kauli yake baada ya kufanyika kwa maombi ya toba na akaamua kumsamehe
-

Kuhusu mauaji mkoani humo amesema yakitokea tena, basi RC mpaka Mtendaji wa Kijiji ataondoka na ikiwezekana Katibu wa CCM wa mkoa huo

huyu mzee ana maneno ya ovyo kuliko wavuvi wa kipemba
 
Utendaji huo afanye kwa walio mpiga risasi mh Lissu.
 
Mechi ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya inayowakutanisha vilabu vikubwa vya Uingereza imekamilika kwa Tottenham kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Manchester City.
Mshambuliaji wa Spurs, Son Heung-min aliamsha furaha za mashabiki wa timu yake katika uwanja wao mpya kwa kufunga goli muruwa katika dakika ya 78.
 
Hata hivyo, ushindi wa Spurs umekuja na machungu pia baada ya mshambuliaji wao tegemezi Harry Kane kutolewa baada ya kuumia mchezoni, na kuna uwezekano asiweze kurejea tena dimbani msimu huu.
Manchester City walipoteza nafasi ya wazi ya kupata goli baada ya penati ya Sergio Aguero kutolewa na kipa wa Spurs Hugo Lloris.
 
Mashabiki wa City bado wanaamini kuwa ushindi mwembamba wa Spurs unaweza kupinduliwa na wachezaji wao kwenye mechi ya marudiano wiki ijayo watakapokuwa nyumbani dimba la Etihad.
Man City wamekuwa wakiangaliwa kwa makini msimu huu iwapo wataweza kuandikisha historia ya kuchukua vikombe vyote vinne wanavyoshiriki msimu huu; Klabu Bingwa Ulaya, Ligi ya Premia, Kombe la FA na Kombe la Ligi.
 
Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino kwa sasa akili yake yote ipo kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo: "Ulikuwa ni mchezo mkali na mgumu. Lakini wapinzani wetu ni Manchester City na kuna mchezo wa marejeano. Tuna furaha kuwa tumeonesha kiwango cha juu. Bado kuna dakika 90 za kucheza."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…