Kiwango tulichokionesha dhidi ya PSG kinatupa matumaini kuwa tunaweza, lakini tunacheza na timu inayopigiwa chapuo zaidi,” amesema Solskjaer.
Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde pia amedai ni ngumu kusema United wameshang’oka.
“Tazama namna walivyofanya jijini Paris (dhidi ya PSG), inabidi utazame tu walichokifanya pale – haya matokeo ya 1-0 bado si ya mwisho,” amesema Valverde.