Pongezi zangu kwa jeshi la Sudan, Natamani hali hii itokee kwenye ile Nchi ya AHADI.
Tatizo kubwa la hawa viongozi wa Afrika ni moja tu. Hata huyo atakayekuja naye utakuta anafanya madudu yale yale na hata mabaya zaidi. Miaka na miaka bara zima liko pale pale hakuna kwenda mbele japo kuna vi exceptions vya hapa na pale (naambiwa pengine Botswana na Rwanda). Tatizo lipo katika mfumo na falsafa ya kijumla. Mwafrika hajui nafasi yake ya kijamii, kimaendeleo na hata kiuchumi katika dunia hii. Hakuna anachofanya bila kuamriwa na wengine. Raslimali nyingi anazo lakini zinawanufaisha wengine. Wanaotawala lengo lao ni kujinufaisha wao na vibaraka wao wachache. Bara karibu lote linanuka ufisadi na ubinafsi wa kutisha wa viongozi.Pongezi zangu kwa jeshi la Sudan, Natamani hali hii itokee kwenye ile Nchi ya AHADI.